ZWAHIRI SASA NI MKUU WA AL QAEDA

Ayman al-Zawahiri, ambaye kwa muda mrefu mno amekuwa msaidizi wa Osama Bin Laden katika kuiongoza Al-Qaeda, na akishikilia nafasi ya pili katika kutoa amri, sasa ataliongoza kundi hilo.
Kiongozi mpya wa kundi la Al-QaedaHayo ni kwa mujibu wa taarifa katika wavuti ya kundi hilo.
Bin Laden aliuawa nchini Pakistan alipopigwa risasi na kikosi maalum kutoka nchini Marekani mwezi Mei.
Kundi la Al-Qaeda limeonya kwamba litaendelea na vita vyake dhidi ya Marekani na Israel chini ya uongozi wa Zawahiri.
Wadadisi wa masuala ya Al-Qaeda wanaelezea kwamba Zawahiri, mwenye umri wa miaka 59, na aliyezaliwa nchini Misri, ni mtu mwerevu sana, lakini hana uwezo wa kuwavutia wafuasi wengi kama alivyofanya Osama.
Baadhi ya wadadisi wanasema yeye ndiye aliyepanga na kuendesha shughuli nyingi zilizohusiana na shambulio la Marekani la 9/11.
Kwa muda wa miaka mingi, msaidizi wa Bin Laden, ambaye atakayefanikiwa kumpata atapokea dola milioni 25 (pauni milioni 15), alitazamiwa kurithi madaraka hayo.
Taarifa iliyotangaza madaraka hayo ilichapishwa katika wavuti ya Al-Qaeda, na kusemekana imetolewa na uongozi wa juu unaotoa amri katika kundi hilo.
"Sheikh Dk Ayman al-Awahiri, Mungu amsaidie, katika kuendelea na uongozi wa kundi", taarifa ilielezea.
Taarifa ilielezea kwamba chini ya Zawahiri, itaendelea na vita vitakatifu vya Jihad dhidi ya Marekani na Israel, "hadi majeshi yote ya wavamizi yanaondoka kutoka ardhi ya Waislamu".
Dk Ayman al-Zawahiri ni mzaliwa wa Misri kutoka familia yenye ushawishi na maarufu.
Maisha yake ya awali alifahamika kuwa na ushawishi wa mafunzo ya Sayyid Qutb, msomi wa Misri anayeaminika na wengi kama Baba wa kuenea kwa Jihad duniani.
Baada ya hapo Zawahiri alihitimu elimu ya dunia na kuhitimu kama Daktari wakati akibuni mfumo wake binafsi wa siku moja kuipindua serikali ya Misri.
Yeye ni miongoni mwa maelfu ya watu waliokamatwa kufuatia mauaji ya Rais Anwar Sadat.
Ilifahamishwa kuwa Zawahiri alinyanyaswa gerezani ambako aliibuka kama msemaji wa wafungwa, akijitokeza kuzungumza kwenye runinga.
Inasemekana kuwa wakati huo Zawahiri alidhalilishwa na hilo kumfanya kugeuka kuwa mwanaharakati wa mfumo wa Jihad kimataifa.
Mwaka 1984, alipoachiliwa, inasemekana alikwenda Afghanistan kujiunga na wapiganaji waliokuwa wakipambana dhidi ya vikosi vya Urusi.
Huko imearifiwa alikutana na Osama bin Laden kwa mara ya kwanza na ndipo walianzisha al Qaeda.
Mke wake na watoto waliuawa katika shambulio la ndege za Marekani mnamo mwaka 2001.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.