Al- Mahmoundi kurudishwa Libya

                                  Aliyekuwa waziri mkuu wa Libya, Baghdadi Al-Mahmoudi 

Rais wa Tunisia, Moncef Marzouki, amesema nchi hiyo haitamuwasilisha kwa mashtaka nchini Libya aliyekuwa waziri mkuu wa Libya, Baghdadi Al-Mahmoudi, bila ya hakikisho kwamba atashtakiwa kwa njia iliyo huru na haki na kwamba atalindwa.

Libya inamsaka Bwana Al-Mahmoudi kwa tuhuma za kutumia vibaya mamlaka.
Al-Mahmudi alitorokea nchini Tunisia punde baada ya Kanali Gaddafi kupinduliwa na anameshikiliwa nchini humo.
Akiwa ziarani mjini Tripoli, Moncef Marzouki, alisema ni ''haki ya raia wa Libya kumhukumu'' waziri mkuu wao wa zamani.
Bwana Mahmoudi alikamatwa nchini Tunisia Septemba mwaka uliopita kwa kuingia nchini humo kinyume cha sheria.
Makundi ya kutetea haki za binadamu zimeiomba Tunisia kutomurudisha nyumbani bwana Mahmoundi, yakisema haki zake za kimsingi zitakiukwa.
Katika hotuba yake mjini Tripoli, Bwana Marzouki alisema kuwa watu wa Tunisia walitaka kukakisha kwa 1000% kuwa haki ya inatendeka, na kwamba kutakuwa na mahakama huru, kabla ya bwana Mahmoudi kurudishwa Libya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA