MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Hamis Ramadhan ‘H-Baba’ amekamilisha kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la Sina Raha, akimshirikisha gwiji wa muziki wa dansi nchini, Ramadhan Masanja, ‘Banza Stone’ Mwalimu wa Walimu.
Akizungumza na Mtandao wa Sufianimafoto, H-Baba, alisema kuwa kibao hicho ni miongoni mwa nyimbo zake 10 zitakazokamilisha albam yake mpya itakayokwenda kwa jina la ‘Shika hapa acha Hapa’ inayotarajia kuingia sokoni mwezi wa tatu mwaka huu.
Aidha alisema kuwa wimbo ambao amemshirikisha Banza Stone, amerokodia katika Studio ya Allan Mapigo, ambapo tayari amekamilisha maandalizi ya kurekodi video ya wimbo huo mwishoni mwa wiki hii.
H-Baba alisema kuwa katika wimbo huo mashabiki wake watarajie kupata vitu tofauti ikiwa ni pamoja na staili mpya na midundo iliyo ‘shiba’ na sauti murua ya Banza Stone, aliyeonyesha uwezo wake katika wimbo huo.
Alizitaja studio alizorekodia nyimbo zake zitakazokamilisha albam hiyo kuwa ni pamoja na KGC Studio, Maneke Studio na Allan Mapigo, zote za jijini Dar es Saam.
Pia alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwamo katika albam hiyo kuwa ni pamoja na, Nipe Kidogo, Shika Kichwa, Kinacho Niumiza, Zaidi yako Wewe na Nimpende Nani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.