MASHINDANO YA MPIRA WA UKUTANI KUANZA KUTIMUA VUMBI ZANZIBAR


Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar.
ZANZIBAR JUMATANO JANUARI 11, 2012. Michuano ya mpira wa ukutani (Squash) ya kutafuta mshindi wa miaka 48 ya Mapinduzi  ya Zanzibar itaanza kutimua vumbi Ijumaa wiki hii Januari 13, 2012 kwenye uwanja wa Polisi Ziwani mjini Zanzibar.
Afisa Habari wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amemkariri Katibu Mkuu wa Chama cha Squash Zanzibar (ZSRA) (Zanzibar Squash Racket Association)  Haji Uzia Vuai, akisema kuwa michuano hiyo itawashirikishi jumla ya wachezaji 30 wakiwemo 15 kutoka Tanzania Bara na wengine 15 kutoka Visiwani Zanzibar.
Vuai amesema michuano hiyo ambayo imekuwa ikifanyika kila mwaka wakati wa sherehe za Mapinduzi, itafungwa Jumapili ijayo Januari 15, 2012 kwenye uwanja wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar na Mohammed Radha.
Amesema mshindi wa kwanza wa michuano hiyo atapata shilingi 200,000, wa pili atapewa shilingi 150,000 na shilingi 100,000 kwa mshindi wa tatu zawadi ambazo amesema zitatolewa na baraza la Michezo la Zanzibar.
Vuai amesema mchezo huo una viwanja viwili tu hapa Zanzibar ambavyo kwa kawaida vinakuwa ndani ya jengo tofauti na viwanja vya michezo mingine. Viwanja hivyo ni kile cha Polisi Ziwani na kiwanja kilichopo kwenye Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
Amewaomba Wananchi mbalimbali wakiwemo wapenzi wa michezo kufika kwa wingi kwenye viwanja hivyo vya SQUASH ili kuona na hata kujifunza sheria na taratibu za mchezo huo.
Vuai amesema kama ilivyo kwa michezo ya ngumi, riadha, kulusha tufe, mkuki ama kuruka juu na chini, ushindi wa mpira wa ukutani nao unategemea sana juhudi za mchezaji  mmoja mmoja wa mchezo huo tofauti na mpira wa miguu ama wa wavu kuwa hata kama mfungaji atakuwa mmoja ama wawili ushindi ni wa timu nzima.
Mwisho
0715 886488, 0784 886488, 0767 886488

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA