MATOKEO KIDATO CHA PILI YATANGAZWA

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Murugo (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam, alipokuwa akitangaza matokeo ya kidato cha pili nchini.

Mkurugenzi wa Shule za Sekondari, Charles Phillemon akifafanua jambo wakati wa kutangaza matokeo hayo ya kidato cha pili. Kulia ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Murugo

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
SERIKALI imesema kwamba kuanzia mwaka huu imerudisha hadhi ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili, hivyo mwanafunzi atakayepata wastani wa chini ya asilimia 30 hataruhusiwa kuendelea na kidato cha tatu, bali ataruhusiwa kukariri darasa mara moja tu.
Imefafanua kuwa mwanafunzi atakariri na kushindwa kufikia wastani wa asilimia 30 ataondolewa ataondolewa katika mfumo rasmi wa elimu. Mbali na hilo imesema ina mpango wa kuurudisha hadhi mtihani wa darasa la nne, hivyo itatoa maelekezo muda si mrefu baada ya kumalizika kwa uchunguzi.
Aidha imeongeza kuwa wazazi na walezi watapaswa kuchangia gharama za za uendeshaji wa mitihani hiyo ikiwemo mingine ya kitaifa ya kidato cha nne na sita kuanzia mwaka huu.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Naibu Waziri wa Elimu, Philipo Mulugo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dares Salaam kuhusu tamko la serikali kuhusu kupandishwa kwa hadhi ya mitihani hiyo na gharama za uendeshaji wa mitihani ya taifa.
“Kuanzia leo tunarudisha hadhi yake,” alisema Waziri Mulugo.
Alisema hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanyika uchunguzi uliofanyika mwaka jana kubaini kuwa moja ya sababu zilizochangia ufaulu duni wa wanafunzi wa kidato cha nne, mwaka 2010 ni kutokana na kuwaruhusu wanafunzi kuendelea na masomo hata baada kushindwa kufikia alama ya ufaulu.
Uchunguzi Ulifanyika baada ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania kuagiza serikali na wadau wengine kufuatilia chanzo cha kushuka kwa ufaulu huo.
Waziri Mulugo alisema ufaulu wa kidato cha pili umekuwa ukishuka kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2010 hivyo kuashiria wanafunzi na walimu kutofanya bidii za makusudi katika kujifunza na kufundisha.
Akizungumzia kuhusu uchangiaji wa elimu wa gharama za uendeshaji wa mitihani ya Taifa alisema uendeshaji wa mtihani umekuwa mgumu kufutia ongezeko la gharama za uendeshaji linaloendana sambamba na ongezeko la idadi ya shule pamoja na wanafunzi mwaka hadi mwaka, ambapo alitolea mfano wa mtihani wa kidato cha pili gharama za zake ni sh. bilioni sita wakati wa kidato cha nne ni sh bilioni 27.9.

Alisema katika mtihani huo wazazi na walezi watakiwa kuchangia sh. 10,000 kwa kila mwanafunzi kwa shule za serikali na zisizo za serikali.
Kwa upande wa mitihani ya kidato cha nne na sita wazazi na walezi watapaswa kuchangia sh .35,000 kwa kila mwanafunzi kwa shule za serikali na zisizo za serikali.
Katika hatua nyingine Waziri Mulugo alisema serikali inatarajia kutangaza ajira za walimu wa msingi na sekondari mwezi huu , na hivi karibuni itatangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha pili.
Hii ni ni mara ya pili kwa serikali kurejesha mtihani wa kidato cha pili mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1999 tangu ulipoanzishwa mwaka 1984.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA