Mfanya usafi akamatwa akimlawiti mtoto msikitini




Tuesday, 24 January 2012 20:40

Hamisi Mwesi, Dodoma
POLISI mkoa hapa inamshikilia mkazi wa Bahi Road, Manispaa ya Dodoma, kwa tuhuma za kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka tisa baada ya kumpa Sh500 ili kumfichia siri.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Zelothe Stephen, alisema mtuhumiwa huyo ambaye ni mfanya usafi wa Msikiti wa Ghazal uliopo eneo la Majengo, alitenda kosa hilo juzi saa 12:00 jioni.

Stephen alisema baada ya polisi kupewa taarifa na wananchi wa eneo hilo, walifika msikitini hapo na kumkamata mtuhumiwa akiwa ndani ya choo cha wanawake alipokuwa akifanyia mtoto kitendo hicho cha kinyama.

“Polisi walijulishwa na wananchi waliokuwapo eneo hilo kwamba mtuhumiwa alimuingiza mtoto huyo kwenye choo cha wanawake na kujifungia ndani, watu waliokuwa jirani na eneo hilo walifuatilia kwa makini ndipo waliposhuhudia mtuhumiwa akimlawiti mtoto huyo na kutoa taarifa polisi,” alisema Stephen.

Alisema mtoto huyo amelazwa Hospitali Kuu ya Mkoa wa Dodoma kutokana na maumivu, kutokana na kitendo hicho na hali yake inaendelea vizuri na uchunguzi juu ya afya yake unafanyika kubaini athari zaidi.

Alisema mama mzazi wa mtoto huyo, alimg’ata sikio la kulia mtuhumiwa huyo kwa hasira na kunyofoka nusu ya sikio lake na kwamba, hivi sasa wanashikiliwa.

Inadaiwa mtuhumiwa amekuwa na tabia hiyo muda mrefu na waumini wa msikiti huo waliwahi kumuonya, baada ya kutiliwa shaka kuhusu kujihusisha na vitendo hivyo ambavyo hawakuwa na ushahidi, ndipo walipoamua kuanza upelelezi dhidi yake.

“Waumini walishamshtukia mtuhumiwa, wakaanza kufuatilia nyendo zake kwani yeye muda mwingi hukaa msikitini kwa ajili ya kufanya usafi, wakati mwingine kutoa adhana kwa ajili ya swala, leo (juzi) amenaswa na mtego baada ya kumtanguliza mtoto choo cha wanawake na yeye kumfuata,” alisema mmoja wa waumini wa msikiti huo.www.mwananchi.co.tz

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA