SOKO LA KISASA LA MWANJELWA JIJINI MBEYA KUENDELEA KUWA KITENDAWILI KUKAMILIKA DESEMBA 2012



Mkurugenzi wa jiji la mbeya Juma Idi
SOKO jipya la Mwanjelwa lililoanza kujengwa Februari 25,2010 ujenzi wa ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Desemba 2012 ambapo ujenzi huo ulipaswa kukamilika Agosti 24,2011.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Juma Iddi alipokuwa akizungumzia masuala mbalimbali na waandishi wa habari .

Mkurugenzi huyo amesema kuwa soko hilo likikamilika liatarajia kuondoa mlundikano wa wafanyabiashara katika masoko ya Sido na Soweto ambapo tangu juzi wafanyabiashara wa masoko hayo waligoma wakilalamikia kupanda kwa ushuru kwa zaidi ya asilimia 50.

Katika suala hilo la kupanda kwa gharama za ushuru kutoka Shilingi 200 kufikia shilingi 300 mpaka 500 kutegemeana na biashara yenyewe, amesema kuwa gharama hizo zipo kisheria na baraza la madiwani liliridhia lakini jana juzi na jana wamekaa na wafanyabiashara hao na kufikia makubaliano ya kulipa Sh 200-300

Amesema licha ya makubaliano hayo, wafanyabiashara wameendelea kugoma waishinikiza uboreshwaji wa miundombinu katika masoko hayo likiwemo soko la Sido ambalo ni chafu jambo ambalo ametolea ufafanuzi kuwa Jiji la Mbeya haliko tayari kufanya hivyo kwasababu masoko hayo si lasmi.

Ujenzi wa Soko la Kisasa la Mwanjelwa unatarajia kutumia Sh Bil 10 ambapo ukijumulisha na gharama za kibenki na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), gharama inafikia Sh bilioni 13.

Kampuni ya Tanzania Building Works TBW ya Dar es Salaam ndiyo inajenga soko hilo.

DESEMBA 2006 Soko la Mwanjelwa jijini Mbeya lililokuwa na ukubwa wa eka 4.7 liliungua. (PICHA, HABARI KWA HISANI YA BLOGU YA MBEYA YETU)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA