TIGO YAWAMWAGIA WASHINDI LAPTOP 48, SH MIL 96

Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Tigo, Alice Maro (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kompyuta ndogo (Laptop), Joyce Mkonyi ambaye amekuwa mmoja wa washindi 48 waliopata kifaa hicho baada ya kushinda promosheni ya "Zamu Yako Kushinda", Dar es Salaam. Katikati ni Ofisa Bidhaa wa Tigo, Pamela Selukindo. (PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)
Mwanate Abdalah wa Mbagala, Dar es Salaam, akikabidhiwa Laptop
Mzee Sylvester Mwagala akipata zawadi yake ya Laptop
Alice Maro wa Tigo (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 4, mteja Grace Munuo
Jackson Ezekiel (kulia0 akipokea hundi ya sh. mil 4




Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Tigo yawazawadia washindi wa promosheni ya “ZAMU YAKO KUSHINDA”

24 Januari, 2012, Dar es Salaam. Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imewazawadia washindi ishirini na nne, kila mmoja shilingi milioni nne, (Tsh. 4,000,000/-) kama washindi wa kwanza wa kila siku ambao wamepatikana katika promosheni inayoendelea ya “Zamu yako Kushinda.” Halikadhalika washindi wengine arobaini na nane wamezawadiwa kompyuta aina ya laptop za Samsung. Washindi wamepatikana katika kipindi cha siku 24, na jumla ya fedha zilizotumika kulipa washindi mpaka leo ni Shilingi za Kitanzania milioni 204.

“Tumeridhishwa na namna ambavyo promosheni inaendelea,” alisema Alice Maro, Meneja Mahusiano wa Tigo. “Bado tunazawadi nyingi za kugawa, kwa hiyo tunapenda kuendelea kuwasihi wateja wetu kushiriki,” alisema.

Baadhi ya washindi wa Tsh. 4,000,000/- ni Juliana Deus (Tabata); Esther Elia (Mbezi Beach); Andrew Mwemezi (Mbeya); Petronila Mtatiro (Ukonga) na Julius Yohana Mlacha (Ubungo).

Baadhi ya washindi wa laptop ni Dini Kaikai (Ilala); Benjamin Jumbe (Dodoma); Mwanate Abdallah (Mbagala); Hezron Chacha Kehongo (Mbezi Beach) na Omar Msuya (Buguruni); George Kessy (Ngara,Kagera).

Washindi wengine wametoka sehemu mbalimbali nchini kama Bukoba, Mwanza, Morogoro, Dodoma, Mtwara, Lindi, Tanga, Moshi, Arusha, Rukwa, Singida and Pwani.

Ili kushiriki mtumiaji wa Tigo anatakiwa kutuma neno “TIGO” kwenda 15571. Gharama kwa kila ujumbe ni Tsh 450. Washiriki wanatakiwa kujikusanyia pointi nyingi ili kujiwekea mazingira mazuri ya kujishindia zawadi. Washiriki pia watazawadiwa zawadi za kutuma ujumbe wa bure kutoka Tigo kwenda mitandao yote Tanzania.

Watumiaji wa mtandao wa Tigo wenye umri chini ya miaka 18, hawaruhusiwi kushiriki. Promosheni hii ni kwa ajili watumiaji wa Tigo watanzania.

Kuhusu Tigo:

Tigo ni mtandao wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu ya hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononikwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengikiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibukaAfrika na Amerika ya Kusini.

Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

Imetolewa na:
Alice Maro • PR-Tigo • Simu 255 715 554501

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA

NOTI MPYA KUANZA KUSAMBAZWA MWEZI UJAO

HUYU NDIYE DKT. NCHIMBI, MAKAMU WA RAIS AJAE