ZIARA YA WAZIRI WA BIASHARA KUTOKA SWEDEN DKT. EWA BJȌRLING KWENYE OFISI ZA NISHATI NA MADINI


Waziri wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja (Mb) akizungumza na ujumbe kutoka Sweden uliomtembelea kwenye ofisi za Wizara ya Nishati na Madini mapema mchana leo. Ujumbe huo uliongozwa na Waziri wa Biashara wa Sweden Dkt. Ewa Bjȍrling na Balozi wa Sweden – Tanzania, Bw. Lennarth Hjelmaker. Nia ya ujumbe huo ni kuangalia fursa za uwekezaji nchini hususan katika nishati jadidifu (renewable energy), mawasiliano ya simu na mitambo. (PICHA NA GREYSON MWASE WA WIZARA YA NISHATI NA MADINI)
Balozi wa Sweden Nchini Bw. Lennarth Hjelmaker akisisitiza jambo mara ujumbe wa Sweden ulipofanya kikao na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. William Ngeleja (Mb.) kwenye ofisi za Wizara mapema leo mchana.
Waziri wa Biashara Sweden Dkt. Ewa Bjȍrling akimkabidhi Waziri wa Nishati na Madini zawadi mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichoshirikisha ujumbe kutoka Sweden na wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini. Nia ya ziara ya ujumbe huo ni kubaini fursa za uwekezaji nchini hususan katika nishati jadidifu (renewable energy), mawasiliano ya simu na mitambo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

ALLY KAMWE AZIMIA KWA MKAPA.

RAIS SAMIA KUZINDUA MKUTANO MKUU WA 79 WA BARAZA LA MICHEZO YA MAJESHI DUNIANI

MIGINGO KISIWA KIDOGO ZAIDI AFRIKA KILICHOGOMBEWA NA UGANDA, KENYA