Aliyemfanyia vurugu Nahodha Mbeya kizimbani
Monday, 07 February 2012 21:21

Stephano Simbeye, Mbozi
HATIMAYE polisi jana walimfikisha mahakamani kijana Aludo Sanga (28), Mkazi wa Kaloleni Tunduma kwa tuhuma za kufanya vurugu kwenye msafara wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha.Katika shtaka hilo, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Amini Rajabu alidai Februari 3, mwaka huu saa 5.50 asubuhi katika eneo la Mwangaza mjini Tunduma, mshitakiwa kwa makusudi alitishia kuharibu mali za Serikali.

Mwendesha mashtaka huyo alidai hali hiyo ilisababisha usumbufu kwa kiongozi huyo wa Serikali aliyekuwa kwenye msafara kwa lengo la kutekeleza majukumu yake ya kikazi.

Baada ya mshtakiwa huyo kusomewa mashtaka yanayomkabili alikana na ndipo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Rahm Mushi aliiahirisha kesi hiyo hadi Februari 21, mwaka huu na kumwachia mshtakiwa.


Hata hivyo hakimu mkazi Mushi aliutaka upande wa mashtaka kuorodhesha mali ambazo wamedai kuwa zilikuwa hatarini kuharibiwa.Wiki Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi alikumbwa na misukosuko akiwa Tunduma ambapo ilielezwa kwamba watu wasiofahamika walimpopoa kwa mawe .

Nahodha alipopolewa hapo Tunduma kwa sababu ambazo hazikuwa wazi ingawa awali ilielezwa kwamba ni kwa sababu ya kutumia magari ya Serikali kwenye mikutano ya CCM.

Naye Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Evans Balama alieleza kwamba kabla ya kupopolewa kiongozi huyo kulikuwapo na vituko vya hapa na pale baina ya vijana wa mji wa Tunduma.

Ilielezwa kwamba baadhi ya vijana walikuwa hawataki kiongozi huyo apite eneo hilo na kwamba vurugu hizo zilizimwa na vijana wenyewe.Lakini baada ya kuzima, msafara ulifika Tunduma na kwamba watu wasiojulikana waliushambulia kwa mawe msafara huo.
Chanzo;Mwananchi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.