BEI YA MAFUTA YA PETROLI YAPAA

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imepandisha bei ya mafuta ya Petroli kwa Sh35 huku mafuta ya taa yakishuka kwa Sh 12. Katika bei elekezi ya Januari 4, lita moja ya petroli kwa bei ya rejereja iliuzwa kwa sh 1,956 lakini, kuanzia jana iliuzwa kwa Sh1,991 kwa lita.

Wakati petroli ikipanda kwa sh 35, bei ya mafuta ya taa ambayo wiki mbili zilizopita ilikuwa ni sh 1,963 sasa imeshuka na yatauzwa kwa sh1,951 huku bei ya dizeli ikabaki kuwa sh 1,903 kwa lita.

Bei hiyo mpya iliyoanza kutumika jana kote nchini, imetokana na mabadiliko ya bei ya soko la dunia, kuimarika kwa thamani kwa asilimia tatu ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola ya Kimarekani.

Kwa mjibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, kanuni mpya ya mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja umesaidia kupunguza ucheleweshaji wa meli mbandarini kutoka siku 15 hadi kufikia siku nne. “Siku 15 ambazo zilikuwa zinatolewa kwenye kanuni ya zamani ya kukokotoa bei hadi kufikia wastani wa siku nne kwa meli kufuatia kuanza kwa mfumo wa uagizaji mafuta kwa pamoja,” alisema taarifa hiyo na kuongeza;

Kupungua kwa siku za ucheleweshaji wa meli bandarini kumechangia kwa kiasi kikubwa kupungua makali ya bei za mafuta katika soko la ndani.

Taarifa hiyo ilifafanua kampuni za mafuta zipo huru kuuza bidhaa za mafuta ya Petroli kwa bei ya ushindani ilimradi bei hizo ziko chini ya bei ya kikomo kama ilivyokokotolewa na kanuni mpya iliyopitishwa na (Ewura).

“Vituo vyote vya kuuzia mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabongo yanayo onekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika,”ilisema taarifa hiyo na kuongeza;

Ni kosa kuuza mafuta bila ya kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja na adhabu itatolewa kwa kituo husika. Kutokana na bei hiyo mpya Petroli kwa Jiji la Dar es Salaam itauzwa Sh1991,Mafuta ya Diseli Sh1977 na mafuta ya Taa Sh1951,Mwanza Petroli itauzwa Sh2141,Diseli Sh2126 na mafuta ya Taa Sh2101.

Katika Jiji la Arusha Petroli itauzwa kwa bei ya Sh2075, Diseli Sh2061 na mafuta ya Taa Sh2035,Mbeya Petroli Sh2098,Diseli Sh2083 na mafuta ya Taa yatauzwa kwa Sh 2058.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.