Mkuu wa Kikosi cha Anga 601 KJ Kizuka , Brigedia Jenerali Joseph Kapwani, ambaye pia ni Base Kamanda wa Vikosi Vilivyopo Ngerengere (aliyeinua mikono ) akimweleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( mwenye suti kulia ) wakati Meneja Mradi wa Maji wa Chalinze,Mhandisi Jeremiah Akonaay , ( kushoto) akisikiliza kwa makini eneo la Ubena Zomozi , yanapojengwa matenki makubwa ya maji yanayayosukumwa na mitambo ya umeme kuekelea Vijiji vitano vya Tarafa ya Ngerengere na kambi tatu za Jeshi,kupitia Mradi wa Maji wa Chalinze.
Meneja Mradi wa Maji wa Chalinze, Mhandisi Jeremiah Akonaay , (kushoto) akitoa ufafanuzi wa kitaalamu wa ujenzi wa matenki ya maji yatakayotumika kusukumwa na mashine kusambaza maji katika Vijiji vitano vya Ngerengere zikiwemo na Kambi tatu za Jeshi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( wapili kulia mwenye suti) juzi ( wa kwanza kulia) ni Mkuu wa Kikosi cha Anga 601 KJ Kizuka, Brigedia Jenerali Joseph Kapwani, ambaye pia ni Base Kamanda wa Vikosi Vilivyopo Ngerengere.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera ( wa pili kushoto) akisalimiana na Ofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) , Luteni Mwajuma Mwakipesile wa Kambi ya 515 KJ akiongozwa na Kaimu Mkuu wa Kikosi hicho, Meja Julius Makena, wakati alipotembelea kuangalia utekelezaji wa miradi ya maji kupitia awamu ya pili ya mradi wa maji Chalinze.
Baadhi ya mafundi wakiunganisha ndondo katika ujenzi wa tanki kubwa la kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya Askari wa JWTZ Kambi ya Kikosi cha Anga Kizuka na familia zao katika Tarafa ya Ngerengere,Wilayani Morogoro, kupitia mradi wa Maji wa Chalinze.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.