HUKUMU YA SAMAKI WA MAGUFULI LEO

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Dar es Salaam leo itatoa hukumu ya washtakiwa katika kesi ya uvuvi haramu, Ukanda wa Kiuchumi wa Bahari ya Tanzania (Exlussive Economic Zone- EEZ), maarufu kesi ya ‘Samaki wa Magufuli’.

Awali katika kesi hiyo ilikuwa na washtakiwa 37, 35 kati yao wakiwa ni raia wa mataifa mbalimbali katika Bara la Asia na wawili wakiwa raia wa Kenya.Katika hukumu ya leo kuna uwezekano mkubwa kushuhudia machozi ya aina mbili, moja ni machozi ya furaha kwa watu ambao hawatapatikana na hatia na kuachiwa huru na machozi ya huzuni kwa watakaopatikana na hatia.

Mshtakiwa wa tisa Hsu Sheng Pao anayedaiwa kuwa mmoja wa mawakala wa meli hiyo, washtakiwa wa 33, Cai Dong Li na wa 34, Cheng Rui Hai huwenda leo wakaamuliwa kwenda kuungana tena na familia zao kwao.

Wengine ni wahandisi wawili wa meli hiyo, mshtakiwa wa 33 na Hai wa 34; na mawakala wawili wa meli hiyo, mshtakiwa wa saba, Zhao Hanquing na mshtakiwa wa tisa Pao.


Pia kuna matumani kwa washtakiwa hao kuachiwa huru baada ya wazee washauri wa Mahakama katika kesi hiyo Magreth Mosi na Bernard Ntumba kuishauri mahakama iwaone hawana hatia na kwamba waachiwe huru.

Wakichambua ushahidi wa upande wa mashtaka na utetezi wa washtakiwa wakati wakitoa maoni yao ya majumuisho ya kesi hiyo, wazee hao walisema upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.

Walisema washtakiwa wa 33 na 34 hawahusiki na mashtaka hayo kwa kuwa wao walikwa ni wahandisi tu wa meli hiyo na kwamba kazi yao ilikuwa ni kuhakikisha meli inafanya kazi.

Kuhusu mshtakiwa wa tisa Pao walisema kuwa upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha ushiriki wake zaidi, mbali kuambatana na mshtakiwa wa saba kuja Dar es Salaam hadi kwa Ofisa wa Polisi.
Lakini mshatakiwa wa kwanza, Hsu Chin Tai ( Nahodha) na mshtakiwa saba, Zhao Hanquing (wakala) wanaonekana kuwa na nafasi finyu ya kuchomoka katika mashtaka hayo.

Pia kuna matumaini hafifu kutokana na wazee washauri wa mahakama kushauri mahakama iwatie hatiani.
Maoni yao kwa mshtakiwa wa kwanza walieleza kuridhika kuwa kulingana na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka dhidi yake kuwa alikuwa akivua katika eneo la Tanzania na bila kuwa na kibali.

“Mshtakiwa wa kwanza alitoa kivuli cha ‘fax’ tena cha meli ya Tawaliq 2 na si Tawaliq1. Wakati akihojiwa na PW8 alikiri kwamba taarifa zilizochukuliwa kwenye GPS zilipokelewa na mtaalamu wa alama,” alisema Mosi.

Kwa upande wake Ntumba alisema ushahidi wa mazingira wa shahidi wa tatu, Msimamizi wa Shughuli za Uvuvi na Sheria za Uvuvi Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Nahodha Ernest Bupamba aliyewakamata washtakiwa hao, unathibitisha mashtaka hayo.
“Pia mshtakiwa Ali Mkotya alikiri kuwa walikuwa wakivua katika eneo la Tanzania bila kibali.

Hata hivyo Jaji hafungwi na maoni ya wazee washauri bali hutoa hukumu kutokana na uzito wa ushahidi wa upande wa mashtaka na utetezi ambao huchambua kwa kuzingatia misingi ya kisheria.

Kutokana na hali hiyo matokeo ya hukumu ya leo yanaweza kuwa tofauti na mtizamo huu.Washtakiwa hao na wenzao walikamatwa Machi 8, 2009 wakiwa samaki tani 293 aina ya Jodari.Mpaka sasa washtakiwa hao wamesota rumande kwa muda wa miaka miwili miezi 11 na siku 15 tangu wakituhumiwa kutenda makosa yanayowakabili.

Washtakiwa hao wamesota rumande kwa muda wote huo baada ya kukosa dhamana licha ya juhudi kubwa zilizofanywa na mawakili wao wanaowatetea Kapteni Ibrahim Bendera na Johna Mapinduzi kuwaombea dhamana mara kadhaabila mafanikio. Cahnzo;gazeti la Mwananchi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.