MADAKTARI NA WAUGUZI WAREJEA KAZINI HOSPITALI YA TAIFA NA AMANA ILALA

Afisa Uhusiano katika hospitali ya taifa ya Muhimbili Aminieli Eligaesha akizungumza na waandishi wa habari leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam (hawapo pichani) kuhusu kurejea kwa huduma za afya katika hospitali hiyo, kufuatia mgomo wa madaktari bingwa na wauguzi uliofanywa katika kipindi cha wiki tatu sasa.
Muuguzi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili akipitia jalada kabla ya kwenda kutoa matibabu kwa mgonjwa katika wodi ya Kibasila ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili leo.

Daktari Charles Some wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akimtoa damu kwa ajili ya vipimo vya matibabu kwa Bi. Upendo Msangi katika wodi ya kibasila. Madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo wamerejea kazini leo (jana) kufuatia agizo lililotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana (juzi) la kuwataka kurejea katika maeneo yao ya kazi.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika hospitali ya amana, wakisubiri huduma za matibabu katika hosptali hiyo, kufuatia kurejea kazini kwa madaktari na wauguzi katika hospitali hiyo mara baada ya mgomo uliodumu katika kipindi cha wiki tatu sasa.
Muuguzi wa kubeba wagonjwa katika hospitali ya Amana Ilala, Mohamed Ally akimpeleka katika chumba wagonjwa, Bi Domitila Haule tayari kupatiwa huduma za matibabu katika hospitali hiyo. Madaktari na wauguzi wamerejea kazini leo kufuatia mgomo waliouitisha takribani wiki tatu sasa.CHANZO BLOG YA FULLSHANGWE

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.