MGAO WA UMEME WAANZA BILA TAARIFA

MAKALI ya mgao wa umeme, mkoani Mara yameanza kimya kimya na sasa unakatwa kwa zaidi ya saa 10.Mpaka sasa wateja wa Tanesco, hawajatangaziwa nini kinaendelea, licha ya uongozi wa shirika makao makuu kutoa taarifa tofauti.

Habari kutoka kwa ofisa mmoja wa shirika hilo alisema siyo mgao huo unatokana na kampuni inayozalisha umeme ya Aggreco kukosa mafuta ya kuendeshea mitambo yake.

“Kampuni hiyo inazalisha zaidi ya megawati 100 zinazoingizwa kwenye gridi ya taifa, tumeambiwa haina mafuta tunatakiwa kupunguza watumiaji. Bunda, Serengeti na Musoma wako kwenye mgao kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 12:00 jioni na hii itachukua muda.

Alisema Wilaya ya Serengeti, waliingia gizani tangu Februari 21 jioni mpaka Februari 22, kwa kile kilichodaiwa kuwa ni uchakavu wa nguzo katika eneo la Bunda na Ushashi na kwamba tatizo hilo limekuwa likijirudia mara kwa mara mvua zinaponyesha.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Edward Ole Lenga alitoa tangazo wakati wa misa ya Jumatano ya majivu katika kanisa katoliki Mugumu kuwapo kwa mgao huo.Baadhi ya wananchi wameendelea kulalamikia uzembe wa Tanesco wa kutorekebisha nguzo chakavu ambazo zinasababisha wakazi wa Serengeti kutokuwa na umeme.

Meneja wa Tanesco mkoa hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo, lakini mameneja wa wilaya walikiri kupokea ratiba za mgao wa umeme kwa mkoa huo.Maneja wa wilaya walisema tatizo la mgao linasababishwa na ukosefu wa mafuta ya kuendeshea mitambo ya kampuni ya Aggreko. Chanzo;Mwananchi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.