MKUTANO WA LONDON WAAZIMIA SOMALIA LAZIMA ISAIDIWE

Mkutano wa kimataifa kuhusu mustakhabali wa Somalia umemalizika mjini London kwa serikali za Marekani na Uingereza zikisema kuwa Somalia lazima isaidiwe kusimama tena na kuwa nchi thabiti.

Waziri Mkuu wa Uingereza , David Cameron, akifunga mkutano huo amesema yalioafikiwa katika mkutano huo ni jinsi ya kumaliza uharamia, kutoa misaada ya kibinadamu, usalama na kulitokomeza kundi la Al Shabaab.

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron aliusifu mkutano huo na kuutaja kama nafasi pekee ya kuigeuza Somalia na kuifanya thabiti na yenye mafanikio makuu.

"Mauritius, Tanzania na Usheli sheli zimekubali kuwapokea washukiwa wote wa uharamia na kuwafungulia mshitaka nchini humo. Somaliland na Puntland na zimekubali kuwapokea na kuwaweka gerezani maharamia wote ambayo tayari wamehukumiwa vifungo katika mahakama mbali mbali duniani. Maharamia wote hawatahurumiwa , wafadhili wao vile vile hawatahurumiwa. Pia tumekubaliana kuhusu kuundwa kwa jopo kazi kuhusu kuzuia ulipaji wa vikombozi kwa maharamia na pia kuzuia uharamia usionekane kama kazi inayoleta utajiri wa haraka haraka", Waziri Mkuu alisema.

Amesema kama hatua ya kuisaidia Somalia, Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zimejitolea kuwapokea maharamia wote wa Kisomali watakao kamatwa na kisha kuwashitaki katika Mahakama za Dar es Salaam.

David Cameron amesema hatua hii ina lengo la kuwabana kabisa maharamia .

Lakini waziri huyo mkuu amesema kuwa njia muhimu zaidi ya kuisaidia Somalia ni kuhakikisha kuna uthabiti wa kisiasa.

Katika mkutano huo ambao kundi la Al shabaab halikualikwa uliapa kukabiliana na kundi hilo na washirika wake wote.

Waziri wa Masuala ya nchi za nje wa Marekani Bi Hilarry Clinton alitangaza kuwa nchi yake haitashirikiana na magaidi na hata makundi ya wanamgambo walioko Somalia.

Hata hivyo kabla ya mkutano huo wa London kuanza msemaji wa Al Shabaab Sheikh Ali Rage aliupuuza mkutano huo na kutoa onyo kwa Uingereza, kutoingilia masuala ya ndani ya Wasomali.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI