MSEKWA, KARUME WAZINDUA KAMPEIN UZINI ZANZIBAR

Vijana wa umoja wa waendeshaji mapikipiki wa chama cha Mapinduzi wakimsindikiza mgombea wa Uwakilishi wa chama hicho junbo la Uzini Mohamed Raza katika uzinduzi wa kampeni wa kuwania kiti cha Uwakilishi Jimbo hilo hapo jana.
Kijana wa chipukizi Zawadi Mbaraka akimvisha Skafu Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Amani Karume baada ya kuingia katika Uwanja wa Mkutano wa CCM kwa ajili ya kuzindua kampeni ya chama hucho huko Uzini wilaya ya kati Unguja.
Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume akibadilishana mawazo na Makamo Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Pius Msekwa huko katika kiwanja cha mpira Uzini wakati wa kuzinduakampeni ya kugombea Uwakilishi wa jimbo hilo.
Wananchi mbalimbali pamoja na wakereketwa wa chama cha CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika huko katika kiwanja cha Uzini Zanzibar kwa ajili ya kumnadi mgombea wa Uwakilishi wa jimbo hilo ndugu Mohd Raza.
Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume akimnadi mgombea wa Kiti cha Uwakilishi jimbo la Uzini ndugu Mohd Raza Huko katika kiwanja cha Mpira Uzini hapo jana .
Mgombea wa Uwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohd Raza akihutubia wananchi pamoja na wanachama wa chama cha Mapinduzi baada ya kutambulishwa rasmi kwa wanachama hao hapo jana Kuliani kwake ni Makamo mwenyekiti wa CCM Zanzibar Amani Abeid Karume.
PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI