Meneja Malipo ya Baada wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Aileen Meena (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu uzinduzi wa promosheni ya kupiga simu za kimataifa ambapo mshindi mmoja atapata zawadi ya safari ya kwenda nchi aliyopiga simu zaidi na washindi wengine 49 watapewa zawadi mbalimbali. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Tigo, Alice Maro. Promosheni hiyo iliyoanza jana kilele chake kitakuwa Aprili 22, mwaka huu. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
Meneja Malipo ya Baada wa Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, Aileen Meena
22 Februari, 2012, Dar es Salaam. Tigo imeanzisha promosheni ya kupiga simu za kimataifa ambapo mshindi mmoja atajishindia safari ya kwenda mahali alipopiga simu zaidi kama vile Canada,China,India,Uingereza na Marekani. Washindi wengine watajishindia begi la Tigo ambalo lina simu aina ya Ideos,tisheti,kibebeo cha ufunguo na kalamu.
Kati ya Februari 22,2012 na Aprili 22,2012,wateja watakao tumia zaidi ya shilingi 1,000 kupiga simu za kimataifa wataingia moja kwa moja kwenye shindano. Jinsi unavyopiga simu za kimataifa zaidi kwa kutumia Tigo ndivyo utakavyojiongezea nafasi ya kushinda.
“Kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana kwenye promosheni zilizopita,tumeamua kuwapa nafasi nyingine wateja wetu wa malipo ya kabla na baada kujishindia zawadi nono”alisema Alice Maro ambaye ni afisa uhusiano wa Tigo. “ Piga simu za kimataifa sasa na ushinde safari ya nje ya nchi”
Kutakuwa na washindi 50 katika promosheni hii. Washindi 49 wa mwanzo watajishindia begi la Tigo litakalokuwa na tisheti,kalamu,kibebeo cha ufunguo pamoja na simu aina ya Ideos smart. Mshindi wa 50 atajishindia zawadi kuu ambayo itakuwa ni tiketi ya ndege na fedha za kujikimu.Mshindi atapewa maelekezo wakati wa mwisho wa maandalizi.
Tiketi ya kurudia itakuwa ni daraja la pili (economy) na itakuwa imelipiwa ikiwa kama sehemu ya zawadi. Tiketi itanunuliwa katika shirika ambalo litachaguliwa na Tigo. Tigo haitahusika na ndege ambazo haijazichagua kutumika katika shindano hili.
Washindi wote 50 watachaguliwa bila mpangilio maalum chini ya uangalizi wa msimamizi kutoka bodi ya michezo ya bahati nasibu. Wateja watajulishwa kupitia namba wanazozitumia kupiga simu za kimataifa. Washiriki wanatakiwa wawe na kitambulisho halali pamoja na pasipoti wakati wanaingia kwenye shindano. Washindi wote watazawadiwa mwisho wa promosheni.
Washiriki lazima wawe na umri wa miaka kumi na nane na kuendelea. Shindano hili ni kwa ajili ya raia wa Tanzania ambao ni wateja wa Tigo.
Kuhusu Tigo:
Tigo ni mtandao wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.
Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepo na Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.
Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz
Imetolewa na:
Alice Maro • PR-Tigo • Simu 255 715 554501

Comments