COCA COLA KUWEKEZA BIL 50 TANZANIA

Coca-Cola Kwanza Managing Director Basil Gadzios talks to the media on the company’s business strategies for year 2012.
Coca-Cola Kwanza’s Director of Public Affairs and Communication Evans Mlelwa talks to the media on the company’s business strategies and plans for year 2012.

Former 1500m world record holder Filbert Bayi who is also the proprietor of Filbert Secondary School tells his success story as an athlete and businessman. He was invited to make a presentation at Coca-Cola Kwanza sales conference held in Dar es Salaam over the weekend.

Former 1500m world record holder Filbert Bayi who is also the proprietor of Filbert Secondary School moves his presentation during Coca-Cola Kwanza sales conference held in Dar es Salaam over the weekend. He was invited to narrate his success story as an athlete and business man. 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Coca-Cola Kwanza kuwekeza Tshs 50bn Tanzania
ZAIDI ya wafanyakazi na maofisa mauzo 200 wa kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola Kwanza kutoka nchi nzima walikutana katika Hoteli ya Kunduchi Beach nje kidogo ya jiji la Dar-es-Salaam mwishoni mwa wiki na kuzindua rasmi msimu wa mauzo wa 2012 wa kampuni hiyo. Wafanyakazi hao  walipata fursa ya kujadili mafanikio na changamoto zilizojitokeza mwaka uliopita na kuweka mikakati ya mwaka huu.
Akihutubia mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Coca-Cola Kwanza Basil Gadzios alisisitiza nia thabiti ya kampuni yake kuendelea kuwekeza nchini Tanzania.
Kampuni hiyo, alisema, itatumia zaidi ya Tsh bilioni 50 katika shughuli mpya na tekinologia mwaka huu. Alisema kwamba kama uchumi wa Tanzania utakua kwa kiwango cha asilimia saba kwa mwaka, kutakuwa na fursa nyingi zaidi za kuendeleza biashara nchini. Vile vile alionyesha nia ya kampuni hiyo kuwekeza katika wafanyazi wake ili kukuza biashara na hivyo kupanua wigo wa ajira kwa Watanzania wengi zaidi.
Gadzios mwenye uzoefu wa zaidi wa miaka 17 katika sekta ya biashara ya vinywaji baridi amejiunga na Coca-Cola Kwanza hivi karibuni baada ya kufanya kazi katika nchi mbali mbali duniani ikiwa ni pamoja na Afrika Kusini, Sri-Lanka na Uganda.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Coca-Cola Kwanza Evans Mlelwa aliainisha changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na kutokuwa na miundombinu mizuri hasa sehemu za vijijini. Hata hivyo alisifu juhudi zinazofanywa na serikali kuendeleza barabara mikoani.
Changamoto nyingine aliyoitaja ni kodi kubwa inayotozwa kwenye biashara ya vinywaji baridi na kuifanya serikali kutokusanya mapato mengi zaidi. Ameshauri kodi ipunguzwe ili kuwezesha kuwa na mauzo makubwa zaidi na hivyo serikali kupata mapato makubwa zaidi.
Mgeni mwaalikwa katika mkutano huo Filbert Bayi, mwanariadha aliyeweka rekodi ya dunia ya  1500m mwaka 1974, aliwataka maofisa mauzo kufanya kazi kwa kujituma, kuwa na nidhamu kazini ili kuwazesha kuvuka mstari wa malengo yao. Kama ambavyo yeye aliweza kuvuka mstari akiwa mshindi,  aliwaomba wafanyakazi hao kukabiliana kikamilifu na changamoto za biashara kwa lengo la kuzishinda na kuendeleza biashara zao.
Bayi aliipongeza Kampuni ya Coca-Cola kwa kuwa katika mstari wa mbele kusaidia maendeleo ya michezo nchini Tanzania na kwa kuchagua Filbert Bayi Secondari kuwa kambi ya kila mwaka kwa wachezaji na viongozi zaidi 600 ambao hushiriki fainali za Taifa za Copa Coca-Cola kila mwaka. Coca-Cola pia inasaidia maendeleo ya mchezo wa kikapu kwa kuendesha kliniki kwa vijana.
Ends…

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.