Live: Tukio zima la Ajali mbaya la basi la Prince Muro iliyo tokea jana Usiku maeneo ya Senjele likielekea Tunduma. Mwendo kasi ndio chanzo cha ajali hiyo mmoja Afariki 14 majeruhi

Basi la Price Muro Baada ya kupata ajali usiku wa kuamkia jana likielekea Tunduma kutokea Dar es salaam.

Likiwa linaonekana baada ya kupinduka

Hivi ndivyo zinavyo onekana Damu na viti kuharibika vibaya baada ya ajali hiyo iliyo tokea jana usiku

Baadhi ya mabaki ya vitu baada ya ajali hiyo jana usiku

Hili Ndilo Gari la mizigo ambalo basi la Price muro lilitaka kulipita, na baadae kushindwa na kupinduka baada ya kukutana na Gari lengine mbele yake


Shimo hili limechimbika wakati wa ajali hiyo ilipo tokea jana usiku

Hapa ndipo Basi la Prince Muro lilipo taka kuingia na kulikwepa gari hili na kupindukia upande wa pili

Muonekano wa gari hili la mizigo ambalo limeharibikia bara barani

Mmoja wa majeruhi ambae alikuwa anatokea Dar es salaam kwenda kuwasalimu ndugu zake Ileje aliye fahamika kwa jina moja tuu la Andendekisye akiwa katika Hospital ya Ifisi Mbeya Muda huu

Baadhi ya Majeruhi walio nusurika katika ajali hiyo wakiwa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea katika matibabu na kutazamwa kama wamepata matatizo yoyote.

Hawa ni majeruhi kati ya wale 14

Mganga mkuu wa Hospitali ya Ifisi Dkt. Mbilinyi akiongea na moja ya majeruhi mapema leo.

Majeruhi ambao wamenusurika katika ajali hiyo mbaya wamesema kwamba dereva huyo alikuwa mwendo kasi tangia walipo fika mikumi, Wameendelea kudai kwamba walimpa onyo mala kadhaa lakini hakuweza kuwasikiliza na akaongeza mwendo kasi zaidi mpaka walipo pata ajali hiyo maeneo ya Senjele kuelekea Tunduma.
Habari kamili itakuja mpaka sasa kuna majeruhi 14 na mtu mmoja amefariki Dunia. (hanzo; Mbeya Yetu Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.