Skip to main content

LOWASSA AHUDHURIA SHEREHE ZA KUSIMIKWA ASKOFU MKUU MPYA WA JIMBO LA IFAKARA

Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kilombero,kabla ya safari ya kuelekea kwenye Sherehe ya Kuzinduliwa kwa Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo.
Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara, Muhashamu Salitaris Melchior Libena akiongoza ibada yake ya kwanza akiwa ni Askofu wa Jimbo Jipya la Ifakara baada ya kusimikwa katika sherehe zilizofaanyika jana Ifakara Morogoro.
Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara, Muhashamu Salitaris Melchior Libena akitoa baraka zake kwa Viongozi wa Serikali waliohudhulia Sherehe hizo za kusimikwa kwake.
Askofu Mkuu Mpya wa Jimbo la Ifakara, Muhashamu Salitaris Melchior Libena akitoa baraka zake kwa wageni mbali mbali waliohudhulia Sherehe hiyo, wakiwemo waandishi wa habari.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akizungumza na baadhi ya waumini wa dini ya Kikristo waliofika kwenye Sherehe hizo, ambapo ameliomba Kanisa Katoliki kuisaidia serikali katika kukabiliana na tatizo la ajira kwa vijana.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili,Mh. Ally Hassan Mwinyi akimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Muadhama Polycarp Kardinali Pengo baada ya kumalizika kwa Sherehe ya Kuzindua Jimbo Jipya la Kanisa Katoliki Ifakara na kusimikwa kwa Askofu Mpya wa Jimbo hilo iliyofanyika jana Ifakara,Mkoani Morogoro.
Mh. Lowassa akibadilishana mawazo na Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea.
Mh. Lowassa akiwapungia mkono wakazi wa Ifakara.
Mh. Lowassa akiwapungia mkono, wananchi kuwaaga wakati akiondoka eneo hilo.
Wanafunzi wakitoa burudani ya kumuaga mh. Lowassa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI