MAWAKALA WA REDDS MISS TANZANIA WAPIGWA MSASA KABLA YA KUANZA KWA SHINDANO HILO

Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, ambao pia ni Waandaaji wa Redds Miss Tanzania 2012, Hashim Lundenga akifungua rasmi semina ya mawakala wa Miss Tanzania 2012 jijini Dar es Salaam iliyoanza leo kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View ya Mbezi jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Redds, kutoka Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL) Victoria Kimaro na Salha Israel Miss Tanzania 2011.


Lundenga amesema  kuwa Kamati hiyo kupitia wadhamini, mwaka huu wamedhamiria  kufanya mapinduzi makubwa katika tasnia ya Urembo nchini na waandaaji pia wamedhamiria kupata warembo bora watakao shiriki shindano hilo la urembo mwaka huu.

Lundenga pia alitoa kaulimbiu ya mashindano hayo kwa mwaka huu kuwa ni “MSHINDI BORA, MWAKILI BORA MWENYE SIFA BORA”
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
 Washiriki wa semina hiyo wakiwa tayari kupata maelekezo mbalimbali kutoka kwa waandaaji pamoja na wadhamini wa shindano la Redds Miss Tanzania 2012.
 Albert Makoye Mkuu wa Itifaki kutoka kamati ya Miss Tanzania akitoa mada katika semina hiyo iliyoanza leo kwenye hoteli ya Girrafe Ocean View iliyoko Mbezi jijini Dar es salaam.
Mawakala wa Kamati ya Miss Tanzania kutoka mikoa mbalimbali na kanda wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa semina hiyo leo jijini Dar es salaam.Chanzo Full Shangwe Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.