MGEJA AIPONGEZA SIMBA

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja akiwa na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, Dar es Salaam(File picture)

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI mstaafu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja ametuma salamu za pongezi kwa timu ya Simba kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Es Setif ya Algeria kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salam.

Mgeja alituma salamu hizo jana alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kuhusu Simba kushinda mchezo huo wa Kombe la Shirikisho uliopigwa juzi.

Alisema ushindi huo ni heshima kwa Simba lakini pia ni sifa kwa Taifa kutangazwa kimataifa kuwa Tanzania ina uwezo mkubwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu ambao una mashabiki wengi duniani.

Mgeja alisema mchezo huo uliofanyika juzi ulikuwa mgumu kwa Simba ikizingatiwa kuwa, Es Setif ni timu kubwa na maarufu barani Afrika.

Alisema ushindi wa Simba ulitokana na uongozi thabiti wa timu hiyo kupitia kwa Mwenyekiti wake, Ismail Rage na wasaidizi wake kwa kufanya maandalizi yaliyowezesha kupatikana kwake.

Akilielezea benchi la ufundi la timu hiyo, Mgeja alisema lilifanya kazi nzito ya kuwaandaa wachezaji na kuzingatia mafunzo hayo kwa kumaliza dakika 90 za mchezo wakiwa na nguvu kama waliyoanza nayo.

Alisema kipindi cha kwa nza cha mchezo huo, Simba ingejitahidi kufanya mashambulizi ya uhakika ingeibuka na ushindi mnono wa zaidi ya mabao matano, lakini si haba, ushindi uliopatikana unastahili kupongezwa na kila mpenda maendeleo na mzalenzo wa nchi yake.

Kutokana na ushindi huo, Mgeja alisema kilichobakia ni kuiombea timu hiyo ifanye vizuri zaidi katika mechi ijayo ya marudiano ambayo itaisogeza Simba katika nafasi ya juu kimichezo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.