MKUTANO WA KITAIFA WA MWAKA WA WAKURUGENZI WAKUU WA WIZARA NA MAKATIBU TAWALA WASAIDIZI KITENGO CHA UTAWALA NA RASILIMALI WATU WAFUNGULIWA RUKWA

Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya, akifungua mkutano wa mwaka wa wakurugenzi wa utawala na rasilimali watu wa Wizara na makatibu tawala wasaidizi Utawala na Rasilimali Watu wa Mikoa uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkoa huo (RDC) jana mjini Sumbawanga. (Picha Hamza Temba-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
utoka kushoto ni Bi. Elizabeth Nyangumi Naibu Katibu Mkuu Hazina, George Yambesi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mkuu wa mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya akifuatilia moja ya mada katikamkutano wa mwaka wa wakurugenzi wa utawala na rasilimali watu na makatibu tawala wasaidizi uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkoa huo (RDC) leo mjini Sumbawanga.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwenye hafla fupi (Cocktail Party) iliyoandaliwa jana usiku na Ofisi yake kwa ajili ya kuwakaribisha wageni waliohudhuria kwenye Mkutano huo. Katika Hafla hiyo vitu mbalimbali viliandaliwa ikiwemo vyakula vya asili ambavyo huzalishwa Mkoani Rukwa kama Maboga, Mihogo, Mahindi Mabichi, na Matunda mbalimbali. Pia walikuwepo Samaki aina ya Migebuka ambao wanapatikana kwa wingi kutoka Ziwa Tanganyika, Mchele (Wali) Mzuri ambao wengine wameubandika jina la Mchele wa Kyella wakati unazalishwa Mkoani hapa pamoja na vinywaji kadha wa kadha. Vilele zilikuwepo Nyama Bora kutoka kiwanda cha SAAFI kinachomilikiwa na Mjasiriamali mzawa na Mbunge Mstaafu Ndugu Chrissant Mzindakaya na Ugali kwa unga unaozalishwa na kiwanda cha Energy Milling cha Wilayani Sumbawanga Mkoani Rukwa. Mkuu huyo wa mkoa aliziomba mamlaka zinazohusika ikiwemo Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kupitia Katibu wake Mkuu George Yambesi kusaidia kuhakikisha kuwa ile kasumba iliyokuwepo hapo kabla ya kuleta watumishi walioshindikana Mkoani Rukwa inaondolewa kwa kuleta watumishi wenye sifa kwani Rukwa Mpya ni tofauti na ile ya zamani. "Rukwa sasa inaruka katika kila sekta" alisema Injiniia Manyanya.
Kutoka kushoto ni Hiporatus Matete Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, George Yambesi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Chrissant Mzindakaya na wadau wengine waliokuwepo kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akigonganisha Glasi ya Whisky na Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Salum Chima viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo jana.
Baadhi ya wageni na wenyeji wakigonganisha glasi katika hafla hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Salum Chima na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Kanali John Antonyo Mzurikwao wakijumuika kwenye Twist na baadhi ya Wajumbe waliohudhuria kikao hicho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.