NHIF ILIVYOENDESHA MKUTANO WA WADAU MTWARA

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia akitoa maelekezo kwa wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakati wa ufunguzi wa mkutano huo jana.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Simbakalia akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Emanuel Humba (kushoto) kabla ya kufungua mkutano.

Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala Beatus Chijumba akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko wa NHIF, Eugen Mikongoti wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa, nyuma ni wadau wa NHIF.
Wadau wa mkutano huo wakifuatilia mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba akigaua fomu zinazojazwa katika Hospitali ya Ndanda kwa wanachama wa Mfuko huo wakati alipotembelea.
Mkurugenzi Mkuu, Emanuel Humba akiwa na wakurugenzi wake wakihakikisha uhalali wa  vitambulisho vya wanachama katika Hospitali ya Ndanda mkoani Mtwara.

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF akijiridhisha uhalali wa vitambulisho vya wanachama kutokana na wimbi la udanganyifu.

Mkurugenzi Mkuu akiwa katika wodi inayolaza wanachama wa Mfuko katika Hospitali ya Ndanda kwa lengo la kuangalia ubora wa huduma wanazopata.


Viongozi hamasisheni wananchi kujiunga CHF-RC

Na Mwandishi Wetu, Mtwara

MKUU wa Mkoa wa Mtwara, Joseph Simbakalia amesema kuwa uendelevu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Mfuko wa Afya ya Jamii unategemea usimamizi wa viongozi serikalini hivyo akawataka viongozi wa Halmashauri mkoani humo kubuni mipango ya kuhakikisha mifuko hiyo inaimarika.

Amesema kuwa Mifuko hiyo ni ya muhimu kwa afya za Watanzania hivyo kila mmoja kwa nafasi yake ahakikishe anatimiza wajibu wake hasa kwa kuhamasisha wananchi kujiunga na mifuko hiyo lakini pia kusimamia huduma katika vituo vya kutolea matibabu ili ziwe bora.

Simbakalia aliyasema hayo jana mjini hapa wakati akifungua mkutano wa wadau wa NHIF uliokutanisha wanachama, watoa huduma, viongozi wa kiserikali, madhehebu ya dini, viongozi wa kisiasa na viongozi wa vyama vya wafanyakazi.

"Ndugu zangu wanasiasa, viongozi wa dini hili suala la afya ni letu sote hivyo tuzungumzeni kwa maslahi ya mwelekeo mmoja ili hatimaye Watanzania waweze kuwa na bima za afya," alisema Simbakali.

Alisema kuwa gharama za matibabu zimekuwa ni ngumu kuzimudu kutokana na upandaji halali hivyo njia pekee ya kuwakomboa wananchi ni kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii hivyo akawataka wadau hao kujadili na kuona ni namna gani itawezesha suala hilo.

"Kuna haja sasa ya kuwepo kwa sheria ili uchangiaji wa Mfuko huu uwe wa lazima, wenzetu wa nchi jirani kama Rwanda wamefanikiwa sana na wakati tukiliangalia hili ni vyema pia tukaweka mikakati ya kuboresha huduma zetu ili wananchi waone umuhimu wake," alisema Simbakalia.

Aidha alitumia mwanya huo kuwataka watoa huduma mkoani humo kutumia lugha nzuri kwa wanachama wa Mifuko hiyo wakati wanapokwenda kupata matibabu kwa kuwa huduma hiyo wameilipia.

Kutokana na hali hiyo, alisema kuwa Uongozi wa Mkoa huo utaendelea kutoa ushirikiano kwa Mfuko huo lakini pia kuzifuatilia Halmashauri katika utendaji wake hasa suala la uhamasishaji kwa wananchi na matumizi sahihi ya fedha zitokanazo na Mfuko huo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba alilisitiza umuhimu wa matumizi ya fedha zitokanazo na Mfuko ambapo alisema kuwa endapo zikitumika vyema zitaweza kupunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la ukosefu wa dawa.

Alisema kuwa lengo la Mfuko ni kuzisadia Hospitali au Vituo vya kutolea matibabu vya serikali kuboresha huduma zake lakini imekuwa kinyume chake kwa kuwa vituo vya  binafsi ndivyo vimekuwa vikipata mapato makubwa kutokana na kutoa huduma bora.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.