Ntaboba wa DRC kumpeleka 'Mke wa Pili' Pasaka

Na Mwandishi Wetu MWIMBAJI nguli wa muziki wa Injili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mwinjilisti Faraja Ntaboba, ni miongoni mwa waliothibitisha kushiriki tamasha la Pasaka litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
 
 Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Msama Promotions, waandaaji wa tamasha hilo, Mwinjilisti Ntaboba amekubali kushiriki.
 
  Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa mwimbaji huyo wa nyimbo za kumsifu Mungu atatua nchini akiwa na albamu yake mpya ya Amenitoa Mbali atakayoitambulisha kwa mara ya kwanza nchini.
 
  Msama alizitaja nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo kuwa ni Nisaidie, Inua Macho, Siku ya Kuinuliwa, Najivunia Yesu, Askari, Kuachwa, Bwana Ameshinda, Kuku na Vifaranga na Samuel. "Ntaboba amesema albamu hii ataitambulisha kwa mara ya kwanza, hivyo ni nafasi nzuri kwa Watanzania kufika kumshuhudia mwimbaji huyo," alisema Msama. Amenitoa Mbali ni albamu ya pili ya Mwinjilisti Ntaboba aliyewahi kutamba na albamu ya kwanza ya Mke wa Pili yenye nyimbo za Yupo Mungu, Mke wa Pili, Mke Mwema, Nikupe Nini, Mwiteni Bwana, Usilie, Mwite Yesu na Hakuna Mwanaume ambazo pia ameahidi kuziimba. Mbali na Mwinjilisti Ntaboba, wengine waliothibitisha kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka ni Rose Muhando, Anastazia Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Atosha Kissava na kundi la Glorious Celebration. Rose Muhando pia atapata fursa ya kutambulisha albamu yake ya nne ya Utamu wa Yesu ambayo haijawahi kuzinduliwa tangu aikamilishe. Albamu ya Utamu wa Yesu inabeba nyimbo saba ambazo ni Utamu wa Yesu uliobeba jina la albamu hiyo, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia. Rose pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawa Sawa. Msama alisema baada ya waimbaji hao kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu. Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane. Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000. Tamasha la Pasaka la mwaka huu pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi sita za Afrika ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Afrika Kusini na Zambia. Pia kutakuwa na kwaya.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.