POLISI, AIRTEL, ROTARY CLUB WAZINDUA MACHAPISHO YA USALAMA BARABARANI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Balozi Kagasheki (wa tatu kutoka kulia mwenye miwani) akishirikiana na viongozi wa Usalama barabarani pamoja na viongozi wa Club ya Rotary ya Dar es Salaam kubandika machapisho ya Usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na Club ya Rotary yenye ujumbe wa kuhakikisha kuwa madereva wanaendesha kwa usalama zaidi bila kutumia siku za mkononi.Kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani  SACP Mohamed Mpinga, muwakilishi kutoka Club ya Rotary Dar es Salaam, Bw. Zainul Dossa pamoja na Bw. Hamza kassongo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Balozi Kagasheki akishirikiana na viongozi wa usalama barabarani akibandika  machapisho ya usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na Club ya Rotary ya Dar es Salaam kulia ni kamanda Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani SACP Mohamed Mpinga, kushoto ni Afisa uhusiano wa kampuni ya Airtel Bi. Jane Matinde akishuhudia zoezi hilo.
Kamanda  Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani SACP Mohamed Mpinga,
akibandika  machapisho ya usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na
kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na  club ya Rotary  yenye ujumbe wa kuendesha +simu =kifo  kuhakikisha kuwa madereva wanaendesha kwa usalama zaidi, ulia ni  ni Afisa uhusiano wa kampuni ya Airtel Bi.Jane Matinde akishuhudia zoezi hilo


Serikali  imesema kutokuwepo kwa sheria ya barabarani inayozuia matumizi ya simu za mkononi wakati wa uendeshaji wa  vyombo vya moto kunachangia kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria madereva ambao waonekana kutumia simu za mkononi huku wakiwa wanaendesha vyombo hivyo.

Hayo yamesemwa na naibu waziri wa mambo ya ndani Balozi Hamis kagasheki wakati wa zoezi la kubandika ujumbe katika magari mbalimbali  unaokataza matumizi ya simu za mkononi wakati wa kuendesha vyombo vya moto.

Ni kweli hadi sasa hakuna sheria inayomkataza moja kwa moja dereva kuacha kutumia simu awapo barabarani lakini naomba wananchi wafahamu kuwa hili linafanyiwa kazi na wafuate maelekezo yalioyotolewa na wadau kama hawa ambayo kiukweli yanatoa elimu ya kupunguza madhara ya ajali za mara kwa mara"

alisema Balozi Khagasheki kwa mujibu wa tathmini ya jeshi la polisi baadhi ya ajali  nyingi zinazotokea barabarani zinatokana na matumizi ya smu za mkononi wakati  wa kuendesha vyombo vya moto hali inayopelekea kuongezeka kwa ajali nyingi na kusababisha vifo  ambavo  vingeweza kuzuilika kwa urahisi.
Balozi kagasheki amesema kuwa upungufu wa kutokuwa na sheria ya kuzuia matumizi ya simu za mkononi wakati  kuendesha gari unapelekea kushindwa kuwachukulia hatua kali madereva ambao wanaonekana kufanya hivyo.

Naye muandaaji wa zoezi hilo Zeinul Dossa kutoka klabu ya Rotary ya jijini dare s salaam pamoja na Jene matinde afisa uhusiano wa kampuni ya smu za mkononi ya Airtel wamesema kuwa zoezi hilo la kubandika ujumbe huo litafikisha ujumbe kwa madereva wengi  pamoja na kupunguza ajali.

Zaidi ya machapisho elfu 5 yametengenezwa kwa ajali ya kubandika pamoja na kusambazwa katika magari mbalimbali  ambayo yatarahisisha kupunguza ajali za barabarani ambazo zinaweza kuzuilika kwa kshirikiana na jeshi la polisi.
Mwisho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.