Rebecca Malope kupamba tamasha la Pasaka

Na Mwandishi Wetu
 
MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope, naye atakuwa miongoni mwa waimbaji watakaopamba tamasha la nyimbo za Injili litakalofanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu tamasha hilo chini ya Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam, Alex Msama, alisema Rebecca amethibitisha kushiriki tamasha hilo.

Msama alisema Rebecca ataungana na waimbaji wa muziki wa Injili kutoka nchi jirani za Zambia, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia na Congo (DRC), Rwanda na Uganda.

Malope atakuwa mmoja kati waimbaji siku hiyo wakiwemo Rose Muhando, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Ephraim Sekeleti, Anastazia Mukabwa, Atosha Kissava na kundi la Glorious Celebration.

Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival inayotamba na albamu yao mpya ya Mtu wa Nne, inatarajia kutumbuiza katika tamasha la Pasaka na Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka DRC.

Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Baada ya kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu.

"Katika tamasha la Pasaka mwaka huu, Rebecca Malope atapata fursa ya kuimba nyimbo mbalimbali zilizomo kwenye albamu zake," alisema Msama.

Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).

"Bado tunaendelea na mazungumzo na waimbaji wengine mahiri wa muziki wa Injili, lakini Rebecca atakuwepo akishirikiana na wengine mahiri kama Rose Muhando, Solomon Mukubwa na wengineo," alisema Msama.

Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.

Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.

Rebecca Malope ni mwimbaji nguli wa Afrika Kusini aliyetamba zaidi kimataifa mwishoni mwa miaka ya 90.

Malope alizaliwa katika shamba la tumbaku Afrika Kusini. Akiwa mtoto, yeye na dada zake walikuwa wakiimba kwaya kanisani.

Alijiunga na kundi la muziki wa injili akiwa binti mwenye umri mdogo, jijini Johannesburg, chini ya mtozi, Zizwe Zakho.

Alianza kutoa albamu yake ya kwanza aliyoipeleka Marekani mwaka 1996 na mwaka uliofuata alisaini mkataba na EMI kisha akatoa albamu ya Free At Last.

Ciao...

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.