SHEIKH APONGEZA TAMASHA LA PASAKA

Na Mwandishi Wetu

WADAU nchini wametakiwa kuiunga mkono Kampuni ya Msama Promotions kwa kuandaa matamasha ya Pasaka, yenye lengo la kusaidia matatizo mbalimbali katika jamii.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Ruvuma, Shekhe Abdul Shakur alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu.

Shekhe Shakur alisema kitendo kinachofanywa na Kampuni ya Msama Promotions chini ya Mwenyekiti wake, Alex Msama ni cha kupongezwa.

Alisema Mungu amempa kipawa kila mtu, hivyo kitendo cha Msama kuandaa matamasha ya injili na kusaidia wajane wasiojiweza, yatima pamoja na kutoa baiskeli kwa walemavu ni jambo la kumshukuru Mungu.

"Ni watu wachache ambao wanaweza kufanya kama kinachofanywa na Msama, naamini kila mtu mwenye mapenzi mema anastahili kuunga mkono kwa kuhudhuria tamasha hilo.

"Nampongeza Msama kwa kuandaa tamasha la kusaidia jamii bila kubagua itikadi za dini... yatima, wajane na walemavu wanaosaidiwa ni ndugu zetu... natoa mwito kwa taasisi nyingine ziige mfano, na ninawatakia heri na fanaka," alisema Shekhe Shakur.

Pamoja na hilo, Shekhe Shakur aliiomba Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo kutanua wigo kwa kulipeleka katika mikoa mbalimbali ili kutoa nafasi kwa wengine kuchangia.

Tamasha hilo linatarajiwa kurindima Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Aprili 8 mwaka huu (mgeni rasmi akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe) na pia litafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 9 mwaka huu (mgeni rasmi akiwa Naibu Spika, Job Ndugai).

Baadhi ya wasanii watakaotumbuiza tamasha hilo ni Rebecca Malope, Rose Muhando, Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Atosha Kissava, Mwinjilisti Faraja Ntaboba, Ephraim Sekeleti, Maryanne Tutuma, kundi la Glorious Celebration na kwaya ya Kinondoni Revival.

Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane.

Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.