TBL YATOA SH. MIL 25 KUSAIDIA MRADI WA MAJI MKOLANI,GEITA

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25, Mhandisi wa Maji Wilaya ya Geita, Daud Sweka kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo za kusaidia mradi wa visima vitatu  vya maji safi na salama ya kunywa kwa wakazi wa Kijiji cha Mkolani-1 wilayani humo hivi karibuni. Katikati ni Meneja Mauzo wa TBL Geita, Issa Msuya.
Mwenyekiti wa mtaa wa Nyamakale, Sizya Mulelemi Mashilungu akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 25 Enock Kangasa, mkandarasi anayatekeleza mradi wa visima vya maji safi na salama ya kunywa kwa ajili ya wananchi wa  kijiji cha Mkolani-1 Geita Mwanza, muda mfupi baada ya hundi hiyo kutolewa na kampuni ya Bia nchini (TBL). Kulia anayeshuhudia ni Meneja Uhusiano wa TBL Editha Mushi.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBl), Editha Mushi (mwenye miwani) akipata maelezo  kutoka kwa mkandarasi, Enock Kangasa (mwenye shati jeupe la mikono mifupi ) ambaye anachimba visima vya maji  katika Kijiji cha Mkolani, Geita, kuhusu 'ring' zinazotumika katika ujenzi wa mradi wa visima vya maji uliofadhiliwa na  kampuni ya TBL  kwa sh. milioni 25. Hafla ya kukabidhi hundi ilifanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki. (NA MPIGAPICHA WETU)

Baadhi ya wananchi wa Nyamakale Mkolani -1  wakiwa na hundi ya sh. milioni 25 walizopewa na TBLa.

Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya msingi Mkolani ambao pia watanufaika na mradi huo maji ya visima ambao TBL imefadhili shilingi milioni 25 kupitia mradi wake wa kusaidia jamii wa Hakuna maji Hakuna Uhai wakishuhudia makabiadhino ya hundi hiyo
Baadhi ya wananchi wa Nyamakale Mkolani -1 wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa TBL  Editha Mushi(hayupo pichani) kabla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 25 kusaidia mradi wa uchimbaji wa visima vya maji kijijini humo jana, katika wilaya ya Geita. (PICHA ZOTE NA MDAU BARTAZAL MASHAKA)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.