TIGO YATOA MSAADA WA KOMPYUTA 37 UDOM

Mratibu wa Promosheni ya Tigo katika Elimu, Edward Shila (kushoto) akikabidhi msaada wa kompyuta kwa Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Profesa Shaaban Mlacha chuoni hapo. Jumla ya Kopyuta 48 zenye thamani ya zaidi ya Sh. mil. 37 zilikabidhiwa na kampuni hiyo kwa ajili ya Kitivo cha Sayansi ya Tiba kwa Jamii. (NA MPIGAPICHA MAALUM)
9 Machi, 2012, Dodoma. Tigo imetoa msaada wa kompyuta 48 kwa chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) kama sehemu ya kuboresha sekta ya elimu na kusaidia matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tecknohama).

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyiaka leo katika chuo kikuu cha Dodoma. Kompyuta zilikabidhiwa kwa niaba ya Tigo na mratibu wa Promosheni na Matukio Bwana Edward Shila. Akizipokea kwa niaba ya chuo,kaimu makamu mkuu mipango, fedha na utawala, Prof. S.A.K.Mlacha ameshukuru Tigo kwa msaada huo na kusema kuwa kompyuta hizo zitasaidia kuboresha mahitaji ya Tecknohama chuoni hapo.

 “Ili tuweze kukabiliana na ushindani duniani,wanafunzi wanahitaji kuwa na uelewa juu ya kompyuta na tecknohama,” alisema Prof. Mlacha. “Msaada huu utawaunganisha na taarifa na tecknolojia kama njia ya kusoma na kupata taarifa ya yale yanayoendelea katika masomo yao,” alisema.

Bw. Shila alisema, “Teknolojia imekuwa ni sehemu kubwa ya maisha yetu, elimu na kazi. Tigo imefurahia kutoa komputa na vifaa vingine kwa viongozi wetu wajao.”

Msaada huu ni muendelezo wa msaada wa vitabu, vilitolewa katika fani ya uhandisi,udaktari na fani nyinginezo ,ambavyo vilikabidhiwa katika chuo kikuu cha Dodoma Desemba mwaka jana  na kuhifadhiwa katika maktaba tano za chuo hicho.

Kuhusu Tigo:

Tigo ni mtandao wa simu za mkononi ya kwanza Tanzania, ilianza biashara mwaka 1994 na ni mtandao wa simu Tanzania wenye ubunifu wa hali ya juu na bei nafuu kupita zote nchini. Tigo ni sehemu ya MillicomInternational Cellular S.A (MIC) na hutoa huduma za simu za mkononi kwa gharama nafuu na inayopatikana maeneo mengi kiurahisi kwa wateja zaidi ya milioni 30 katika masoko 13 yanaoibuka Afrika na Amerika ya Kusini.

Msingi wa mafanikio ya Tigo ni uzingatiaji wa mikakati mitatu ambao,ni Gharama nafuu, Uwepo na  Upatikanaji .Tunajenga dunia ambapo huduma za simu ni za bei nafuu, zipo na zinapatikana kila mahali na kwa wote. Hii inahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma bora zaidi kwa bei nafuu kuliko zote katika mikoa yetu 26, Tanzania Bara na Zanzibar.

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz

Imetolewa na:
Alice Maro • PR-Tigo  • Simu 255 715 554501

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.