Washabiki wa mpira Misri wakasirika

Mapigano yamezuka katika mji wa Port Said nchini Misri na kijana mmoja amekufa, baada ya timu ya mji huo kupigwa marufuku kwa miaka miwili kufuatia ghasia za mwezi Februari, zilizouwa watu zaidi ya 70.
Mamia ya washabiki wa klabu hiyo ya al-Masry walipambana na askari wa usalama walipozingira jengo la serikali, kulalamika juu ya timu yao kupigwa marufuku.
Inaarifiwa kuwa polisi walitumia moshi wa kutoza machozi na kufyatua risasi hewani.
Adhabu hiyo ya klabu ya al-Masry kukatazwa kucheza kwa miaka miwili, imetokana na ghasia zilizozuka katika uwanja wa timu hiyo ilipopambana na al-Ahly ya mjini Cairo.
Wamisri wengi wanawalaumu askari wa uslama kwa kutozimua ghasia za mwezi Februari.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.