UZINDUZI WA KIOTA CHA MARAHA CHA CITY SPORTS & LOUNGE WAWA GUMZO DAR

 Mashabiki wa Chelsea wakishangilia ubingwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo uliopo Jengo la Hifadhi, katikati ya Jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Uzinduzi huo ilifanyika wakati wa mechi ya fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA) kati ya Chelsea na Bayern Munich.
 Mashabiki wa Chelsea wakishangilia ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) ndani ya mgahawa huo. Kushoto ni Julius Kihampa ambaye ni Mhariri wa Michezo wa gazeti la Jambo Leo na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Quality Group, Christina Manongi 'Sinta'.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mgahawa wa kisasa wa City Sports & Lounge, Juma Pinto (kushoto), akimtambulisha Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba wakati wa hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo uliopo Jengo la Hifadhi, katikati ya Jiji la Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo. Uzinduzi huo ilifanyika wakati wa mechi ya fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA) kati ya Chelsea na Bayern Munich
Wateja wakihudumiwa nyama choma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mgahawa huo
                                                 Gadna akielezea utaratibu wa sherehe za uzinduzi
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Benchmark Rita Poulsen (kulia) na  Msanii Sara Kaisi 'Shaa' walikuwa miongoni mwa wateja waliohudhuria hafla hiyo.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa mgahawa huo, Juma Pinto  (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa mgahawa huo, Benny Kisaka (wa pili kushoto) wakiwa na wateja Evans Aveva  (kushoto) na mteja mwingine wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wateja miongoni mwao akiwemo mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), wakishuhudia mechi ya fainali ya UEFA ndani ya mgahawa huo.
 Wateja wakishuhudia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) kati ya Chelsea na Bayern Munich wakati wa uzinduzi  wa mgahawa huo wa kisasa uliosheheni luninga kila mahali.
 Mashabiki wa chelsea wakishangilia ubingwa wa Kombe la UEFA.
 Wateja wakicheza muziki wa disko uliokuwa ukiporomoshwa ndani ya ukumbi huo
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athuman Nyamlani (katikati), akielezea sheria za utabiri wa wateja kuhusu matokeo ya mechi ya Chelsea na Bayern munich. Kulia ni Mchambuzi wa  wa masuala ya soka, Eddo Kumwembe na Mkurugenzi wa mgahawa huo, Benny Kisaka.
Vodacom Miss Tanzania 2011, Salha Israel akiwa miongoni mwa wateja waliohudhuria ufunguzi wa mgahawa wa City Sports & Lounge, Dar es Salaam juzi. Kutoka kulia ni William Malecela, Mkuu wa Itifaki wa Miss Tanzania, Albaert Makoye na Ofisa Masoko wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Mabakila.
Wadau wa burudani, Grace Michael (kushoto) na Grace Kingarame hawakukosa hafla hiyo ya ufunguzi wa kiota hicho cha maraha kilichopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.