JK aonya kampuni kuendeshwa kifamilia

RAIS Jakaya Kikwete amesema kampuni nyingi nchini zimeshindwa kuendelea kutokana na kuendeshwa kifamilia, badala ya kuuza hisa na kumilikiwa na umma. Akizindua Karakana ya Ndege ya Kampuni ya Precision Air jana, Rais Kikwete alisema kampuni nyingi nchini zinatakiwa kubadili mfumo wa uendeshaji.

“Watanzania wanaimiliki Precision Aair kwa asilimia 59, huu ni mfano wa kuigwa kwa sababu ziko kampuni nyingi zimebaki kuwa za familia tu,” alisema Kikwete. Hata hivyo, Rais Kikwete alisema suala la hisa kwenye sekta ya anga bado ni biashara ambayo watu wengi hawajaielewa vizuri tofauti na sekta zingine kama benki. Alipongeza shirika hilo kwa kutengeneza karakana hiyo na kuitaka iwe na viwango vya hali ya juu vitakavyokidhi matakwa ya kimataifa.

“Tuache viwango vya kibongobongo, tukilipua tutahatarisha ustawi wa ndege na kampuni zitakazokuwa zinatumia karakana hii,”alisema. Pia, alitaka Wizara ya Uchukuzi na ile ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kujenga chuo cha ufundi wa ndege nchini.

“Siku hizi sijui hata wanajifunzia wapi... tunaona wanaruka tu walikojifunzia wanajua wenyewe,”alisema Rais Kikwete. Naye Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa shirika hilo, Michael Shirima alisema hadi sasa wana mtaji wa dola 2 milioni za Marekani na kwamba, wana ndege 12 huku wakimiliki tisa kati ya hizo.

Shirima alisema mradi wa kutengeneza karakana hiyo ulibuniwa mwaka 2006, ili kutengeneza ndege zao wenyewe badala ya kupeleka nje. Alisema awali walikuwa wakipeleka ndege zao kwa matengenezo makubwa Botswana na Malawi, hatua iliyosababisha kutumia gharama kubwa. Pia, alisema usafiri wa ndege nchini ni ghali kutokana na sheria zilizopo ambazo nyingi zinazuia uhuru wa biashara.

“Tunaomba Serikali ituunge mkono kwa kununua hisa ili tupanuke zaidi, kwa sababu sisi ni Shirika la Umma,” alisema Shirima. Mwenyekiti huyo alisema wanatarajia kuongeza ndege nyingine tano na kwenda kimataifa zaidi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.