MAJAMBAZI YATIKISA CHATO

WATU 11 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za moto na za kijadi, wamevamia Kijiji cha Kibehe, wilayani Chato,Geita na kupora fedha, simu za mikononi na kujeruhi watu watano.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana baada ya majambazi hao kuteka kaya zaidi ya tano, kabla ya kufyatua risasi kadhaa hewani na kuwafanya wananchi washindwe kutoka ndani ya nyumba zao.


Baadaye, majambazi hao walitumia mapanga na marungu, kuwajeruhi baadhi ya wananchi wakati wakiwashinikiza kusaimisha fedha na simu za mkononi.


BaaWatu walioshuhudia tukio hilo, Mussa Limbe na Inocent Moshi, walisema katika tukio hilo lililodumu kwa zaidi ya saa mbili, majambazi walimteka na kumweka chini ya ulinzi wao, mwalimu wa Shule ya Msingi Kibehe.

Kwa mujibu wa mashuhuda hao, baadaye, mwalimu huyo alitumika katika kuwatembeza majambazi hayo katika kaya za watu wenye fedha.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Geita, Leonard Paul, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba polisi wanaendelea kuwasaka watu hao.


Paul aliwataka wananchi kutoa taarifa zitakazowawezesha polisi kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani. Chanzo; Mwananchi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

GSM ARIDHIA UJENZI WA UWANJA WA YANGA JANGWANI

WACHEZAJI YANGA WAGOMA KABISA KUFANYA MAZOEZI LEO, LWANDAMINA AIBUKA PEKE YAKE SHAMBA LA BIBI

DKT. MAJULE AMFANYIA MAPOKEZI MAKUBWA BALOZI WA CHINA NCHINI

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

Wasifu wa Kizza Besigye

HERSI KWENDA KUSOMA TENA CHUO KIKUU CHA OXFORD UINGEREZA