*MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL MGENI RASMI TUZO ZA WASANII BORA 2012 WA MUZIKI WA ZANZIBAR HAFLA YAFANA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Heshima msanii mstaafu wa muziki wa Taarab, Mwanacha Hassan Kijole (65) wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel.Hafla hiyo ilifanyika jana usiku katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa redio ya Zenji Fm, Mohamed Seif Khatib (kushoto) ni Mkurugenzi wa Biashara wa Kampuni ya Zantel, Zanzibar, Mohamed Baucha.
 Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa sanaa, waliohudhuria hafla hiyo.
  Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa sanaa, waliohudhuria hafla hiyo.
 Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Zakhia Bilal, akiwa ni miongoni mwa wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
 Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa sanaa, waliohudhuria hafla hiyo.
 Mkurugenzi wa redio ya Briz Fm, bi. Mariam, akimkabidhi Tuzo ya kuwa msanii bora wa Kike wa muziki wa Afro Pop, Msanii Baby J, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika jana katika   Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Abdallah Mwinyi Mkuu, akimkabidhi Tuzo mwanamuziki wa kundi la Taarab la Zanzibar One Modern Taarab, Saada Nassor, baada ya kuibuka mshindo kwa kuwa Msanii bora wa Kike wa mwaka wa muziki wa Taarab ya Kisasa, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika jana  katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
 Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa redio ya Zenji Fm, Mohamed Seif Khatib, akimkabidhi Tuzo msanii, Rukia Ramadhan, aliyeibuka mshindi kwa kuwa mwimbaji bora wa mwaka wa Taarab Aslia, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za  Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.
 Mwakilishi wa Benki ya NBC kwa niaba ya Meneja wa benki hiyo, Asya Mohamed, akimkabidhi tuzo ya kuwa na Studio bora ya mwaka 2012, Juma Mkuyumba 'Mk Records', wakati wa hafla hiyo jana.
 Ombeni Swai, kutoka Kampuni ya Scannad ya jijini Dar es Salaam, akimkabidhi Tuzo mmoja kati ya wasanii waliofanya vizuri mwaka 2012. 
 Abubakar Liongo,  akimkabidhi Tuzo msanii aliyefanya vizuri mwaka 2012, katika muziki wa Hip Hop, Sabri Mshimba 'Chaby Six, wakati wa hafla hiyo. 
 Msanii Isma, akishambulia jukwaa wakati wa hafla hiyo.
 Kundi la Dansi la Young Dancers, likishambulia jukwaa kwa burudani.
 Msanii aliyeibuka kidedea katika kategoli ya Muziki wa Afro Pop, Rashid Khalfan Ali 'Dogo Fanni' akitembea kwa madaha kuelekea jukwaani kukabidhiwa tuzo yake wakati wa hafla hiyo.
 Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa sanaa, waliohudhuria hafla hiyo.
 Mwakilishi wa Jimbo la Raha Leo, Salim Nassor, akimkabidhi tuzo ya Msanii Bora Chipukizi wa mwaka, msanii Emma Score, wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za washindi wa Tuzo hizo za Wasanii bora wa muziki wa Zanzibar wa mwaka 2012, zilizodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.

Picha ya pamoja baada ya zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi wa tuzo hizo. Picha na Sufiani Mafoto Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.