MWENYEKITI REDDS MISS TANZANIA KUIPATIA KWAYA STUDIO


 Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Prashant Patel (kushoto) akiwa na Rais wake Hashim Lundenga


DAR ES SALAAM, Tanzania

MWENYEKITI wa Kamati ya Miss Tanzania, Prashant Patel, ameahidi kujenga studio ya kisasa ya kurekodi nyimbo kwa wanakwaya wa kanisa Katoliki la Mtakatifu Kamili la Yombo Kiwalani jijini Dar es Salaam.

Ahadi hiyo, aliitoa mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa albamu yao, inayojulikana kwa jina la Kitimtim.

Alisema, studio hiyo itakuwa ni suluhisho katika kurekodi nyimbo bila usumbufu wowote kwa wana kwaya hao.

Aliongeza kuwa, kwaya hiyo ina mahitaji mengi, ambayo yanaweza kupatiwa uvumbuzi taratibu.

Aidha, Patel alitoa sh milioni 1 kwa ajili ya uzinduzi wa video ya albamu hiyo yenye nyimbo mbalimbali, ikiwemo; ‘Nimepata rafiki’, ‘Kuishi kwangu’, ‘Kitimtim’, ‘Eh Mungu uimarishe amani’.

Awali, Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya sherehe hizo, Edwin Laurint, alisema, kwaya yao ina changamoto nyingi,  ikiwemo ya usafiri.

Alisema, licha ya kukosa basi, pia wanahitaji sh milioni 24 kwa ajili ya kuendeleza mahitaji yao na malengo.

Katika uzinduzi huo, kwaya hiyo iliweza kutambulisha rasmi video ya wimbo wa Kitimtim kwa mara ya kwanza.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.