SIMBA WAWAPANIA VIBONDE PORTS LEO


MABINGWA wa Tanzania, Simba leo watashuka dimbani kuwakabiri vibonde Ports kutoka Djibouti katika mchezo wa pili wa Kundi A utakaochezwa kwenye Uwanja wa taifa Jijini Dar es Salaam.

Mchezo mwingine wa kundi hilo utakaofanyika mapema utawakutanisha vinara wa AS Vita Club ya DR Congo dhidi ya URA ya Uganda, mchezo unaotegemewa kuwa na upinzani mkali kutokana na timu hizo mbili kushinda kwenye michezo yake ya kwanza.

Simba itaingia uwanjani ikiwa na lengo moja la kusaka ushindi mnono dhidi ya Port iliyofungwa mabao 7-0 na Vita Club katika mchezo wa kwanza ili kuwatuliza mashabiki wake kama ilivyokuwa kwa mahasimu wao Yanga walioshinda 7-0 dhidi ya Wau-Salaam jana.

Katika mechi ya kwanza ya michuano hiyo Simba ilichapwa mabao 2-0 na URA ya Uganda.

Akizungumzia mchezo huo kocha wa Simba, Milovan Cirkovic alisema anategemea kufanya mabadiliko madogo katika kikosi chake baada ya kugundua mapungufu katika mchezo uliopita.

Alisema moja ya makosa aliyoyabaini katika safu ya ushambuliaji ni kushindwa kutumia vizuri nafasi wanazozipata na amerekebisha tatizo hilo.

"Ingawa sijapata mchezaji wa kuziba nafasi ya Emmanuel Okwi na Patrick Mafisango, ndio maana unaona sehemu ya ushambuliaji inakuwa na tatizo, nimeifanyia kazi na ninaendelea kutafuta mchezaji wa kudumu kuziba pengo la Okwi," alisema Milovan.

"Baada ya mchezo dhidi ya URA niliona makosa pia kwenye upande wa kuzuia, hasa mipira ya juu. Tatizo hilo nimelifanyia kazi kuhakikisha halijirudii tena, nina imani kubwa ya kusonga mbele baada ya mchezo wa leo,"alisema Milovan.

Naye nahodha na kipa wa Simba, Juma Kaseja alisema mapungufu ya mabeki yaliyojitokeza katika mechi dhidi ya URA hayatajirudia tena.

"Mabeki hawakujipanga vizuri, lakini kocha amelifanyia kazi tatizo hilo, wote tumemwelewa na kujipanga vizuri kwa ajili hilo lisitokee tena,"alisema Kaseja.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.