TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


YAH: TAARIFA KUWA BAADHI YA WALIMU ‘WAMEIKACHA’ CWT SIYO YA KWELI

Gazeti la Nipashe la tarehe 9 Julai 2012 ukurasa wa pili iliandikwa taarifa yenye kichwa; Baadhi ya walimu ‘waikacha’ CWT. Maelezo haya siyo ya kweli maana walimu hawajajitoa (kuikacha) CWT na wale walioshawishiwa wajitoe walishindwa maana waliahidiwa na viongozi wa UMET kuwa mara ukiandika barua ya kujitoa makato yako ya 2% yatasitishwa jambo ambalo haliwezekani. Kusitishwa kwa makato ni suala la kisheria kuwa Chama kinapofikisha zaidi ya nusu ya wafanyakazi wa sekta hiyo waliobakia wanatakiwa kukatwa 2% ya huduma kwa chama (Union Service charge) kwa sheria Na 10 ya Vyama Huru vya wafanyakazi ya 1998 na huduma ya wakala (Agency fee) kwa sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini namba 6 ya 2004. Hakuna sheria inayoruhusu mwanachama kujitoa chama na kufuta makato na hii ni sheria ya Bunge siyo matakwa ya CWT, maana huwezi kuwa unafaidi matunda kwa jasho la wenzako (Free rider).

Idadi ya wanachama wa UMET iliyotajwa kwenye gazeti la Nipashe hiyo si ya kweli, mfano mkoa wa Mbeya kuwa na wanachama 3,641 si kweli maana wanachama wa CWT Mbeya ni 13,833 kati ya walimu 16,934 hivyo wangekuwa na kiasi hicho (3,641) Mbeya isingetawalika ki-CWT . Hizo takwimu za wanachamwa UMET wanzipataje wakati hawajasijiriwa? Je, wanachama wao wanawajuaje? Kw mujibu wa sheria ya Ajira na Mahusaiano Kazini ya 2004, Ili uwe mwanachama wa chama cha wafanyakazi chochote lazima uwe umejaza fomu inayoitwa TUF 6 yaani (Trade Union Form Number 6) na baada ya hapo wanachama wanajazwa kwenye daftari la wanachama kwa fomu namba 15. Je, hao UMET wanachama wao wamewapataje kwama siyo propaganda na uzushi? Nadhani wanashindwa kutofautisha kati ya wanachama na hisia za kuwa na washabiki. UMET wanadhani kila anayemshabikia nyoka aliyeuawa anampenda nyoka kumbe wengine wanataka kuona ukubwa na aina ya nyoka aliyeuawa.Wajaribu kuchanganua mambo kwa mapana zaid.

Kumekuwa na taarifa za upotoshaji kwa wanachama na walimu wenye mapenzi mema na CWT yao juu ya vitega uchumi vya CWT. Kimsingi CWT inakitega uchumi kimoja tu yaani jengo la ‘Mwalimu House’ lenye ghorofa kumi lililoko Ilala Boma. Jengo hilo ni la kupangisha na mapatoi yake ni kati y ash, 35 hadi 40 milioni kwa mwezi. Aidha, kuanzishwa kwa kampuni ya walimu TDCL (Teachers’ D eveolpment Company Limited) wala lengo lake si kufanya biashara bali ilianzishwa kwa lengo la kupata nafuu ya kodi katika uwekezajiambayo ni sera ya CWT. Mapato na matumizi ya fedha zote za Chama yanakaguliwa kila mwaka na mkaguzi wan je fedha toka Kampuni inayotanmbuliwa na kuwasilishwa kwa Msajili wa vyama vya wafanyakazi. Chama kisipowasilisha ukaguzi wake wa fedha kinafutwa. Aidha, mwanachama hazuiliwi kuuliza mapato na matumizi ya fedha za chama kwenye ofisi za CWT hakuna siri yoyote.

Kwa mantiki hiyo, maelezo ya UMET ni ya kupotosha walimu na inaonyesha viongoizi wake wanatumiwa na serikali ili kuwagawa walimu wasidai maslahi bora wakati huu ambapo CWT kimetangaza mgogoro na serikali. Natoa wito kwa walimu kuwa makini na makundi haya yanayotumiwa na serikali pamoja na propaganda na vitisho mbalimbali vya serikali. Wakati ukifika wa mgomo tuungane wote bila woga wala kulinda vyeo vyetu serikalini kama ualimu mkuu, uratibu, ukuu wa shule, n.k. tudai maslahi bora kwa walimu wa kizazi hiki ili tuwe tayari kutoa elimu bora kwa watanzania. Walimu wawe macho na kila namna yoyote ya kuwagawa au kuwachonganisha na CWT wasahau kuidai serikali maslahi bora. Kila mwalimu anahitaji maslahi bora.

Nawatakia kazi njema na afya tele.

MSHIKAMANO DAIMA! NA NDIO MKOMBOZI WETU

Mwl. Kasuku Bilago
Katibu CWT Mkoa
Mbeya

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.