USHIRIKIANO KATI YA TANZANIA NA CHINA KUENDELEA KUZINUFAISHA SEKTA ZA KILIMO, NISHATI, VIWANDA NA BIASHARA.

Balozi wa China nchini Tanzania Lu Younqing (kushoto) akifurahia jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema nchi yake itaendelea kuimarisha ushirikiano kati yake na Tanzania katika Nyanja za Kilimo, Nishati, Biashara na Viwanda. Kulia ni mshauri wa masuala ya Sayansi na Teknolojia wa ubalozi huo Bw. Liu Dong.
Baadhi ya wafanyakati wa ubalozi wa China nchini Tanzania wakifuatilia mkutano kati ya balozi wa nchi hiyo  Lu Younqing na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
 Dar es salam.
 
Tanzania itaendelea kunufaika katika nyanja za kilimo, Biashara, uwekezaji wa nishati, Biashara na viwanda kutokana na uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizi.
 
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salam na Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lu Youqing alipokutana  na waandishi wa habari kuelezea mafanikio yaliyopatikana kutokana na ushirikiano uliopo kati ya nchi hizi kwa mwaka 2010 na 2012.
 
Balozi Lu amesema sasa kiwango cha biashara kimeongezeka kutokana na juhudi mbalimbali zilizofanyika kuondoa vikwazo  vilivyokua vikiwakabiri
wafanyabiashara kutoka Tanzania.
 
Amesema kiwango cha uwekezaji kwa mwaka 2011 nchini Tanzania kinafikia dola za kimarekani milioni 339  huku akifafanua kuwa kuna makampuni mbalimbali yaliyowekeza nchini Tanzania kwenye kilimo , nishati, shughuli za usafiri wa meli na miradi ya televisheni kwa mfumo wa digitali.
 
Amefafanua kuwa tayari China na Tanzania zimekubaliana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo ukiwemo mradi wa uzalishaji wa nishati ya umeme wa Mchuchuma utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha kiasi cha megawati 600.
 
Balozi Lu ameongeza kuwa Tanzania na China kwa muda mrefu zimekuwa zikishirikiana katika sekta ya biashara huku akitoa mfano wa maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam yaliyomalizika hivi karibuni katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salam.
 
Amesema ushiriki wa China katika maonyesho hayo ni ishara tosha ya ushirikiano wa kibiashara kati ya Tanzania na China kwa kuwawezesha wananchi wa Tanzania kuona bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa nchini China zikiwa na ubora na gharama nafuu.
 
“Nakiri wazi kuwa maonyesho yaliyomalizika katika viwanja vya sabasaba yaliwawezesha wafanyabiashara kutoka China kuja Tanzania kuonyesha kazi wananzozifanya, hiyo ni ishara tosha ya ushirikiano, watanzania waliweza kuona na kujipatia bidhaa kutoka China kwa gharama nafuu huu ni mfano tu wa ushirikiano uliopo”
 
Kuhusu fursa za biashara ya kimataifa zilizopo amefafanua kuwa anatambua misingi na kanuni zinazozingatiwa na kuongeza kuwa biashara zote lazima zifanyike kwa usawa huku akifafanua kuwa watanzania kupitia Kilimo kwanza wataweza kuzalisha mazao na kuyaongezea thamani kisha kuuza bidhaa zitokanazo na mazao hayo na kujipatia kipato.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.