Wabunge wa Simba wawachapa kwa penalti 3-2 wa Yanga, Uwanja wa Taifa

Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM), Nape Nnauye akisalimiana na mshambuliaji wa timu ya Wabunge wa Simba, Joshua Nassari kabla ya pambano lao leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi cha Wabunge wa Simba kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya pambano lao na Wabunge wa Yanga katika mchezo maalum wa kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi. Wabunge wa Simba wamewachapa wa Yanga kwa mikwaju ya penalti 3-2.
Kikosi cha Wabunge wa Yanga kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya pambano lao na Wabunge wa Simba katika mchezo maalum ulioandaliwa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa ajili ya kuchangisha fedha zitakazotumika katika ujenzi wa Mabweni ya wanafunzi.

Nahodha wa timu ya Wabunge wa Simba, Amosi Makalla (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na nadhodha wa Yanga pamoja na waamuzi wa mchezo huo.
Mshambuliaji wa timu ya Wabunge wa Simba, Zitto Kabwe (kushoto), akichuana na beki wa timu ya Wabunge wa Yanga, Michael Kadebe katika mchezo wa kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni ya wanafunzi vijijini.
Mshambuliaji wa timu ya Wabunge wa Simba, Zitto Kabwe akimtoka beki wa Wabunge wa Yanga, Abdallah Haji.
Joshua Nassari wa timu ya Wabunge wa Simba akimtoka beki wa timu ya Wabunge wa Yanga, Michael Kadebe katika mchezo huo.
Wachezaji wa akiba wa timu ya Wabunge wa Yanga, wakifuatilia mchezo huo.
Benchi la ufundi la timu ya Wabunge wa Yanga likiongozwa na kocha mpya wa Yanga, Tom Saintfiet. (Picha na Francis Dande)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.