DK BILAL AFUNGA MAONESHO YA NANENANE DODOMA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi kikombe Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Fatuma Salum Ally, baada ya Halmashauri ya Wilaya hiyo kuwa kuwa mshindi wa jumla katika maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo Agosti 8, 2012, wakati alipokuwa akifunga maonyesho hayo  katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mmoja kati ya wajasiliamali wa vikundi vya wakulima, wakati alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo Agosti 8, 2012 katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili wakati walipowasili kwenye Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma leo Agosti 8, 2012 kwa ajili ya kufunga rasmi maonyesho hayo .Picha na Muhidin Sufiani-OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati alipomwakilisha Rais Jakaya Kikwete, kufunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nanenane yaliyomalizika leo Agosti 8, 2012 katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha Tuzo aliyokabidhiwa kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Rais katika kusimamia na kuendeleza Kilimo Kwanza, wakati Makamu alipokuwa akifunga rasmi maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima Nane Nane katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma leo Agosti 8, 2012. Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.