DK ULIMBOKA AREJEA NCHINI NA KUSEMA

Nimepona, naweza kufanya kazi zangu kama kawaida.
Apokelewa kwa shangwe na Madaktari wenzake, wanaharakati na wananchi wa kawaida walia machozi ya furaha.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Stephen Ulimboka amewasili leo alasiri majira ya saa 8.15 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam akitokea Afrika Kusini alikopelekwa na madaktari wenzie kutibiwa.
Dk. Ulimboka, alipelekwa huko, Julai mwaka huu, baada ya kutekwa,kuteswa na watu wasiojulikana na hatimaye kutupwa Msitu wa Mabwepande Juni 28, mwaka huu.

Kwenye Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, alilakiwa na madaktari wenzie, wanaharakati na wananchi ambao baadhi yao walipomuona waliangua kilio.
Gari lililombeba Dk. Ulimboka, lilisukumwa na watu hao lililopokuwa linaondoka Uwanja wa Ndege.
Uongozi wa Jumuiya ya madaktari ulisema kuwa umefurahi kumuona kamanda wao amerudi salama salimini na kwamba hali hiyo imechochea ari ya kuendeleza mapambano ya kudai haki yao.
Aidha uongozi huo, umesema, utaandaa taarifa maalumu juu ya tukio hilo, na kuzungumza na vyombo vya habari.

Daktari Ulimboka hapa akiwasihi ndugu zake pamoja na Madaktari wamwache azunguimze kidogo na waandishi ili akate kiu yao baada ya kusubiri uwanjani hapo kwa muda mrefu, lakini ndugu na madaktari hao wakionekana kipinganaye na kumtaka aende akapumzike na taarifa zote zitolewe baadaye, hata hivyo alizungumza na waandishi baada ya mvutano wa muda kidogo.
Hapa sasa anazungumza na waandishi na kuwashukuru watanzania wote kwa kumuombea na madaktari wenzake kwa kumuunga mkono
Hapa sasa anaondoka huku akishangiliwa na madaktarfi wenzake kwa nyimbo na vigeregere. Huku mwenyewe akitokwa na machozi pamoja na baadhi ya ndugu zake na madaktari walionekana pia wakitokwa na machozi.
Makubdi ya watu waliojitokeza kumlaki wakiwa kwenye mlango wa kutokea abiria wakimsubiri majira ya saa 7:00 hadi saa 8:15 alipowasili.
Ndugu zake waliposhindwa kujizuia walipomuona Dk Ulimboka na kumfuata ndani kabla hajatoka nje.
Hapa anashindikizwa kwenda kwenye gari.

akipanda kwenye gari.
gari likisukumwa na madokata pamoja na wanaharakati bila kuwasahau wananchi wa kawaida.
Gari likiondoka eneo la Uwanja huo wa Ndege wa Kimatgaifa wa Julius Nyerere.Picha kwa hisani ya Raha za Pwani Blog

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.