MASHINDANO YA SOKA YA KUWANIA NG'OMBE,MBUZI,KONDOO NA JOGOO YAANZISHWA

Mratibu wa mashindano ya soka ya vijana katika Mji Mdogo wa Utete, Rufiji, Mtangashari Mtolia (kulia), akielezea jinsi mashindao hayo yatakavyoendeshwa katika kiutano uliofanyika mjini Utete jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa kamati ya mashindano hayo, Uwesu Omari na Mweka Hazina Khamis Mninge. Washindi wa michuano hiyo itakayoanza Agosti 26, mwaka huu,watazawadiwa ng'ombe, mbuzi, jogoo na kondoo. (PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)

 Na Richard Mwaikenda,Utete,Rufiji

MASHINDANO ya kugombea zawadi ya ng'ombe, yatakayoshirikisha timu 16 za vijana yanatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu katika Mji Mdogo wa Utete, wilayani Rufiji, Pwani.

Akizungumza na Jambo Leo mjini Utete juzi, Mratibu wa mashindano hayo yatakayojulikana kama Vijana Cup, Mtangashari Mtolia, alisema kuwa lengo la michuano hiyo ni kuibua na kuvikuza vipaji vya soka kwa vijana wilayani humo.

Alisema kuwa wachezaji hao watakaokuwa na umri kati ya miaka 20 na 25, watatoka katika Kata tatu zinazounda mji huo wa Utete, ambazo ni Utete, Chemchem na Ngarambe.

Mtolia alisema, mashindano hayo yatakayofanyika kwa mwezi mzima kwenye Uwanja wa Azimio mjini Utete, yataendeshwa kwa mtindo wa makundi na baadaye Ligi mpaka atakapopatikana bingwa.

Alisema, kuwa timu bingwa itazawadiwa ng'ombe dume, wa pili atazawadiwa mbuzi wawili beberu, mshindi wa tatu mbuzi mmojja na jogoo halafu wa nn ataambulia kondoo.

Aliwataja wadhami wa michuano hiyo kuwa ni Mjumbe wa Baraza la Michezo Taifa (BMT), Kamishna Msaidizi wa Polisi, Jamal Rwambow na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mdogo wa Utete, Masoud Jah.

Mahindano hayo yatakayofunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Nurdin Babu yataongozwa na kamati , ambayo wajumbe walitajwa kuwa ni; Uwesu Omari (Mwenyekiti), Mtengashari Mtolia (Katibu),  Khamis Mninge (Mhazini), Athuman Sule, Ali Mopele na Mohamed Kipepe.


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.