Rais Museven ampa Kiprotich Sh 200 mil


KAMPALA, Uganda
BINGWA wa mbio za marathoni katika michezo ya Olimpiki, Stephen Kiprotich jana aliteka kwa muda hisia na mawazo ya wakazi wa jiji la Kampala baada kupewa mapokezi ya pekee kwa aina yake alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Entebe.

Sehemu kubwa ya viongozi mbalimbali wa serikali wakiongozwa na Waziri wa Elimu na Michezo wa Uganda, Jessica Alupo walijazana uwanjani kumlaki shujaa huyo aliyerejea na medali ya dhahabu.Baada ya kupokelewa, Kiprotich alipelekwa katika hoteli ya kifahari mjini Entebe kwa ajili ya kupumzika.

Kabla ya kwenda kupumzika Kiprotich alizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo kuwaeleza furaha yake ya kushinda medali hiyo ya dhahabu.

Saa nne asubuhi Kiprotich alipelekwa Ikulu ya Uganda iliyopo Entebe na kupokelewa na rais wa Uganda ambaye alitumia muda huo kumpongeza kwa kuipeperusha vizuri bendera ya Uganda katika michezo ya Olimpiki.

Pia rais Mseveni alimpa Kiprotich hundi ya Sh200milioni za Uganda na kuahidi kujenga nyuma ya vyumba vitatu kwa ajili ya wazazi wake.

Kiprotich alikunywa chai na rais Mseveni na baada ya hapo alielekea katika ofisi za Baraza la Michezo la Uganda zilizopo huko Lugogo.

Tangu Jumapili iliyopita, ambapo Kiprotich alishinda mbio za marathon (km 42), jina la Kiprotich limekuwa likitajwa sehemu mbali na Waganda na wamekuwa wakimsubiri kwa hamu.

Wakati huohuo, kampuni ya AS Vision Group wachapishaji wa gazeti la New Vision la Uganda waliendesha zoezi la kukusanya fedha kwa watu na makampuni mbalimbali ya Uganda kwa ajili ya kumpatia Kiprotich, ambapo mpaka jana walikuwa wamekusanya kiasi cha Sh300 milioni za Uganda huku lengo la kampuni hiyo ni kukusanya kiasi cha dola 500,000.

Katika siku ya Jumapili, Vision walikusanya kiasi cha Sh250milioni za Uganda, Jumatatu Sh18milioni na Jumanne 25 milioni, ambapo zoezi hilo linaendelea.

Kazi ya kumchangia Kiprotich itaendelea kwa muda wa wiki moja na watu binafsi na makampuni yote yatakayochanga fedha watatangazwa na kampuni na Vision Group.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.