TFF YASOGEZA KIPINDI CHA USAJILI WA TIMU ZA LIGI KUU NA LIGI DARAJA LA KWANZA


SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limesogeza mbele kipindi cha kuwasilisha usajili kwa klabu za ligi kuu na ligi Daraja la kwanza msimu wa 2012/2012 hadi Agosti 15 mwaka huu.Awali zoezi hilo lilikuwa likamilike leo. 
 
Katibu Mkuu wa TFF , Angetile Osiah alisema kwamba marekebisho hayo yanatokana na mkanganyiko uliojitokeza na kusababisha baadhi ya vilabu kuchelewa kuwasilisha majina. 
 
Alisema kutokana na mabadiliko hayo, muda wa siku saba za kuwasilisha pingamizi utakuwa kuanzia Agosti 15 hadi Agosti 22, 2012, kabla ya kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji kukutana kupitisha usajili Agosti 24 hadi Agosti 25, 2012. 
 
Alisema klabu zinatakiwa ziwasilishe usajili pamoja na mikataba ya wachezaji kama kanuni zinavyotaka na usajili wa kwanza utahusu timu za vijana walio na umri chini ya miaka 20. 
 
Katibu hiyo pia amezitaka klabu zote zinazoshiriki ligi kuu na ligi daraja la kwanza kuwasilisha majina ya viwanja zitakazovitumia kwa ajili ya msimu ujao. 
 
“Pia klabu husika ziwasiliane na vyama vyao vya mikoa ili viwasilishe maombi ya kutumia viwanja hivyo kwa mechi za ligi kuu na ligi daraja la kwanza msimu mpya wakati zikisubiri ratiba kutangazwa”, alionmgeza Osiah

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.