USALAMA WA KANDA MUHIMU KWA KUIMARISHA MTANGAMANO WA EAC

Na Mwandishi wa,EANA
Arusha, Agosti 21, 2012 (EANA)—Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa,Dk. Julius Rotich, amevitaka vyombo vya ulinzi na intelijensia vya kanda kuhakikisha kuwa Afrika Mashariki inabaki kuwa kanda salama kwa wote.

Akihutubia kikao cha viongozi waandamizi wa vyombo vya usalama vya EAC mjini Kigali, Rwanda Juzi, Dk.Rotich alisisitiza kuwa ugaidi, madawa ya kulevya na usafirishaji haramu wa binadamu vimekuwa vikiibuka kwa haraka kama uhalifu sugu unaovuka mipaka ya nchi wananchama.

‘’Changamoto zinazotolewa na ugaidi, moja kati ya tishio kubwa katika kanda inasisitiza umuhumu wa sekta hii katika kuhakikisha kwamba watu wake wanasafiri kwa uhuru na salama.Suala hili lina umuhimu unafanana na vita dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu ambapo kanda hii inatumika kama njia kuu ya kupitishia,’’ alisema katika hotuba ambayo nakala yake ilipatika kwa Shiriki Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA).

Alisema sekta ya usalama katika kanda ya EAC ni muhimu katika utekelezaji wa mafanikio wa Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja, kama hatua za kwanza na pili za mtangamano wa kina ambao hatimaye unalenga katika kufikia shirikisho la kisiasa.

“Usafirishaji wa silaha na madawa ya kulevya na matokeo ya mapambano na vyombo vya usalama inamaanisha uhitaji wa uangalizi wa karibu wa upatikanaji wa usalama wa bidhaa katika kanda, limebaki kuwa jukumu la msingi sekta hii,” alisema.

Takribani watu 50 walikutwa wamekufa katika kontena la mizigo nchini Tanzania hivi karibuni. Walikuwa wanasadikiwa kuelekea Afrika ya Kusini, eneo ambalo limekuwa kivutio kwa Pembe ya Afrika kwenda kutafutia maisha bora.

Dk.Rotich pia alibaini kuwa kanda ina makundi mbalimbali yenye wajibu wa ulinzi na usalama na hivyo ni muhimu kuweka utaratibu wa kuratibu shughuli hizo kuepuka kurudia jukumu ambalo limeshafanywa na chombo kingine.

Kuhusu utegemezi wa ufadhili, afisa huyo wa EAC alisema kuwa nchi wanachama zinatakiwa kuanza kuunga mkono mipango ya usalama. ‘’Asilimia 95 ya mipango yetu ya sekta hii inategemea wafadhili. Lazima tuliangalie upya hili ili tuwe na mipango yetu ya kiulinzi endelevu ambayo tunaimiliki wenyewe,” alisema.

Mwenyekiti wa kikao, David Njoka, kutoka Kenya alisema kuwa sekta hiyo inahitaji kuangaliwa kwa umakini kutokana na umuhimu wake kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa Afrika Mashariki.

‘‘Ulinzi na Usalama vinaambatana na malengo yetu kwa manufaa ya Afrika Mashariki,” alisisitiza.

Mkutano huo utafuatiwa na kikao cha wakuu wa polisi wa nchi wanachama na Kamati ya Uratibu (inayojumuisha Makatibu Wakuu).

Mkutano wa mawaziri utafanyika Agosti 27 katika sehemu hiyo hiyo.

Baraza la sekta ya Usalama kwa nchi wanachama wa EAC linajumuisha mawaziri wanaohusika na mambo ya ndani, shughuli za maafa, uhamiaji, polisi, magereza, intelijensia na udhibiti wa ugaidi.

mm/fk/ni

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.