WABUNGE WAISIFU APRM

Na Mwandishi Wetu,Dodoma
Wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akisema kuwa Serikali imetekeleza kwa kiwango cha juu mchakato wa tathmini ya utawala bora nchini (APRM) na kulipongeza Baraza la usimamizi la Taifa la APRM wabunge kadhaa wameshauri taasisi hiyo iimarishwe zaidi.
Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje mwanzoni mwa wiki hii, Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo alisema taasisi ya APRM ni muhimu sana katika kuisaidia nchi kujitazama kiutawala bora na kufanyiakazi changamoto husika.
“APRM inafanyakazi nzuri sana kwa nchi yetu lakini iimarishwe zaidi. Kwa mfano Baraza la Taifa la Usimamizi limekuwa madarakani kwa muda mrefu sasa kwa nini wasiwe wanabadilishwa kama inavyofanyika kwa wajumbe ambao ni wabunge ambao hubadilika kila baada ya miaka mitano?” alihoji mbungu huyo.
Kwa upande wake Msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni, Ezekia Wenje (Chadema) aliishauri Serikali kulipa michango inayofikia dola 800,000 ambayo haijalipwa makao makuu ya APRM kwa miaka minane ili kuifanya Tanzania ionekani machoni mwa nchi nyingine za Afrika na duniani kuwa ina nia ya dhati kisiasa na mpango huo.
Katika hotuba yake Wenje pia alisisitiza kuwa ni vyema kukawa na sera ya kulibadilisha baraza la Taifa la usimamizi la APRM ili kulipa hadhi Baraza hilo liweze kuwa na mawazo mapya.
“Baraza la sasa la APRM limekuwepo tangu mwaka 2006. Ni vyema kukawa na sera ya kubadilisha wajumbe wake kila baada ya miaka mitano ili kuleta akili mpya ndani ya Baraza hilo,” alishauri.
Akieleza utekelezaji wa majukumu ya Wizara na taasisi zilizoko chini yake, Waziri Membe alisema utekelezaji wa mchakato wa APRM unaendelea vyema.
“Mchakato wa APRM umeendelea vyema ambapo mwaka huu Serikali ilipokea timu ya wataalamu kutokamakao makuu ya APRM kwa ajili ya kuihakiki ripoti yetu,” alisema.
Aliongeza kuwa kazi yatathmini ya utawala bora nchini ilifanyika kwa uadilifu mkubwa na akatambuakazi iliyokuwa ikifanywa kwa weledi na bodi ya APRM. Bodi ya APRM kwa sasainaongozwa na Prof. Hasa Mlawa.
APRM ni Mpango wa Barala Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora ulioasisiwa mwaka 2003 na tayari mpaka sasa nchi 34 za Afrika zimeshajiunga. Hapa nchini taasisi hiyo imepewa dhamana ya kukusanya maoni ya wananchi kuhusu hali ya utawala bora ilikuisaidia Serikali kufanyiakazi changamoto zinazojitokeza na ilianzishwa mwaka 2007 baada ya nchi kusaini mkataba mwaka 2004.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.