ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII DK. RASHID WILAYANI RUFIJI

 Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Dk. Seif Rashid  (Kulia)  akisalimiana na akina mama wa Kijiji cha Mtanza baada ya kumalizika kwa mkutano na wananchi wa eneo hilo wakati wa  ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge pamoja na kuwaeleza majukumu mengine aliyonayo sasa ya unaibu waziri.
Dk Rashid akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Mtanza jimboni humo juzi. Kulia ni Diwani wa Kata ya Mwaseni, Athuman Mbange (CUF) na kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtanza.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji, Dk. Seif Rashid  (wa pili kukushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa Kata ya Mwaseni, akikagua maendeleo ya ujenzi wa chumba cha darasa wa ziara ya kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kuwa mbunge pamoja na kuwaeleza majukumu mengine aliyonayo sasa ya unaibu waziri.
Bibi Fatuma Mazengo akiangua kilio mbele ya waziri alipokuwa akieleza jinsi mkwe wake na mjuu wake walivyouawa kinyama na Askari wa Wanyapori katika Hifadhi ya Mbuga ya Selou mpakani mwa kiji cha Mloka, Rufiji. Watu hao waliuawa walipokwenda kuvua samaki katika ziwa la Mzizizmia kwa ajili ya kitoweo
Akina mama wa Kijiji cha Mibuyu Saba  wakisikiliza kwa makini hotuba ya Waziri

Mkazi wa Kijiji cha Mtanza, Yusufu Nyamgumi, akihoji kwenye mkutano kitendo cha Diwani wao, Athuman Mbange (CUF) kutokuwa na tabia ya kuwatembelea kujua matatizo yao, (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA)


NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII, DK. RASHID ATEMBELEA GHAFLA KITUO CHA AFYA CHA NYAMINYWILI, RUFIJI
 Na Peter Ambilikile

KITUO cha Afya cha Nyaminywili kilichopo Kata ya Mwaseni, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani,kinakabiliwa na ukosefu wa wafanyakazi pamoja na vitendea kazi kunakofanya shughuli nyingi za kiutendaji kuteteleka siku hadi siku.

Kituo hicho kimekuwa kikipokea wagonjwa 30 kwa siku ambapo wengi wao wamebainika kuumwa malaria, kifua kikuu na magonjwa ya kuhara kunakosababisha na unywaji maji ya kisima bila kuchemsha.

Aidha kuna changamoto za kiutendaji zinazoendana na wananchi wengi kutofahamu umuhimu wa kituo cha afya kilichopo karibu hali inayosababisha  kutotoa ushirikiano unaotakiwa kwa wafanyakazi wa kituo hicho.

Wakizungumza mbele ya Naibu Waziri ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji Dk. Seif Rashid, Kaimu Mganga Mkuu wa kituo hicho, Abdala Wattanga alisema kituo hicho kina mtabibu mmoja ambaye yupo katika mafunzo akisaidiwa na wasaidizi watatu.

Rashid alisema kutokana na hali hiyo imekuwa ni vigumu kuhudumia wangonjwa kwa wakati kunakofanya baadhi ya watumishi katika hosipitali hiyo kutokwenda likizo na kufanya kazi zaidi au kukesha katika kazi kunakotokana kuwepo na wangonjwa wa dharura.

Naibu waziri wa afya aliyesimama kwa ajili ya kukagua kituo hicho alipatwa na mshangao baada ya kuelezwa kuwa wagonjwa katika kituo hicho hulazimika kuchangia sh. 30.000  fedha za mafuta ili waweze kupeleka mgonjwa katika hospitali ya utete akihitaji matibabu.

Dk. Rashid ambaye hakupendezwa na kauli hiyo alisema inakuwaje mtu mgonjwa kumogezea ghalama na kuhoji kama wanapata fedha toka halmashauri husika ambapo kaimu mganga mkuu alikiri kupata fedha kidogo zisizotosheleza hata kupeleka mgonjwa mmoja.

kutokana na maelezo hayo Dk. Rashid alisema atalifuatilia zaidi tatizo hilo katika halmashauri ambapo alipendekeza vituo vyote nchini viweze kuwa na akiba ya mafuta yasiyopugua lita 100 mpaka 200 na kuweza kusaidia wagonjwa wa dharura kama akina mama wanaoweza kuhitaji upasuaji na bajeti hiyo ni ndani ya mwezi mmoja.

Naye dereva wa gari ya wagonjwa aliyejitambulisha kwa jina la Hamisi Mkasi alitoa shutuma kwa baadhi ya ndugu za wangonjwa wanaowasindikiza wagonjwa wakati wa dharura kama vile kujifungua na kulazimika kwenda Hospitali ya Utete na wanapochangia mafuta huambatana na mashariti lukuki.

Masharti hayo ni pamoja na mgonjwa pindi anapolazwa Utete kutakiwa kumrudisha yule alimpeleka na kuweza tena kumfuata anapotoka hospitalini kwa mafuta yale yale alioyatoa ya sh.30,000  ambapo kutoka Nyaminywili hadi Utete ni kilomita 100.

Aidha Dk. Rashid alishitushwa na kitendo cha kuwepo na watu katika kijiji hicho kuvamia sehemu ya eneo la kituo hicho kwa ajili ya kujenga msikiti ambapo hata hivyo alielezwa kuwa mtabibu mkuu wa wilaya aliingilia kati suala hilo kwa kushirikiana na ofisi ya tarafa.

Matatizo mengine yanayokikabili kituo hicho ni pamoja na upungufu wa vifaa vya hosipitali kama vile vitanda,glovu,mabomba ya sindano ambapo Wakala wa Dawa wa Serikali (MSD) imetupiwa lawama kwa kutokuwa makini katika kuleta dawa kama walivyoagiza kulingana na mahitaji ya kituo chao.

"mnaweza mkawa mnaagiza dawa za malaria au kifua lakini utashangaa mnaletewa maboksi ya kondomu au mara nyingine mnaletewa dawa zilizopita muda wake"alisema Kaimu Mganga, Wattanga na kuongeza kuwa MSD kwao imekuwa ni kero kunakochangia kuzorota kwa shughuli nyingi za kiafya kituoni hapo.

Pia Wattanga alimuomba Naibu Waziri wa Afya Dk. Rashid kuruhusu madaktari wanaofanya kazi pembezoni mwa nchi kupatiwa posho maalum ya kuwawezesha kumudu maisha na kufanya kama motisha ya kufanya kazi sehemu hizo.

Pia Dk. Rashid aliwataka wauguzi kuwa wavumilivu wakati huu ambapo serikali inapitia upya posho za usumbufu kazini na kuongeza kuwa hata yeye wakati akifanya kazi katika hosipitali ya utete alikumbana na vikwazo vingi ikiwemo kukosa nyumba ya kuishi pamoja na mazingira duni ya kufanyia kazi.

Kituo cha afya cha Nyaminywili kinatarajiwa siku za karibuni kuongezwa au kupanuliwa huduma zake kwa kuongeza chumba maalum cha upasuaji na kufanya vijiji vinavyozungukwa na kata hiyo kufaidika na huduma hiyo.



mwisho









 












Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI