.Lampard aiokoa England

Mkwaju wa penalti wa Frank Lampard katika dakika za mwishomwisho uliiwezesha England kuondoka na angalau pointi moja katika mechi ya kufuzu kushirikishwa katika michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ukraine, katika uwanja wa Wembley.

Yevgeni Konoplianka aliweza kufunga bao la kusisimua katika kipindi cha kwanza na kuiwezesha Ukraine kupata nafasi ya kuongoza, hadi zikiwa zimesalia dakika tatu mechi kumalizika, juhudi za England hatimaye zilipata ufanisi.

Mchezaji wa zamu Danny Welbeck ambaye alibadilisha mchezo tangu alipoingia, alishuhudia juhudi zake zikizimwa kwa njia isiyo halali na Yevgeni Khacheridi, na kutokana na adhabu iliyotolewa ya penalti, Lampard, kama ilivyo desturi, akiwa makini na mtulivu, aliweza kufunga bao la kusawazisha.

Baadhi ya wachezaji mahiri wa England hawakuweza kushiriki katika mechi hiyo, na ilikuwa ni pigo kubwa zaidi baada ya nahodha Steven Gerrard naye kuamriwa na mwamuzi kuondoka uwanjani, baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya manjano, na inamaanisha mchezaji huyo sasa ataikosa mechi nyingine ya kufuzu katika uwanja wa Wembley mwezi Oktoba, wakati timu yake itakapopambana na San Marino.

Ilikuwa dhahiri kwamba matokeo hayo yalimridhisha meneja wa England Roy Hodgson, ambaye ilikuwa wazi uso wake ulionyesha baada ya timu yake kuwakosa wachezaji mahiri kupitia maradhi na majeraha, ilikuwa ni afadhali kuondoka na hiyo pointi moja badala ya kuondoka pasipo lolote, na ilikuwa ni kinyume na Ijumaa iliyopita wakati walipoinyeshea Moldova magoli 5-0 huko Chisinau.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI